» » Trump ashutumu ufichuzi wa ripoti dhidi ya mwanasheria mkuu

Image captionRais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumu ripoti iliofichuliwa kinyume cha sheria kwamba mwanasheria wake mkuu alijadili maswala ya kampeni na mjumbe mmoja wa Urusi.

Gazeti la Washington Post lilitoa maelezo kuhusu mikutano ambayo mwanasheria mkuu Jeff Sessions alifanya na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergey Kislyak.

Bwana Sessions awali alikuwa amekana kufanya mazungumzo hayo kuhusu kampeni.

Mamlaka ya Marekani inachunguza kuhusu hatua ya Urusi kuingilia kati uchaguzi huo.

Trump ajutia kumteua mwanasheria mkuu Jeff SessionsDonald Trump amfuta kazi mwanasheria mkuuMaseneta wamuidhinisha mwanasheria mkuu wa Trump

Huduma ya kijasusi inaamini kwamba Urusi iliingilia uchaguzi huo ili kumsaidia Trump kushinda .

Urusi imekana na Trump anasema kuwa kampeni yake haikushirikiana na Urusi.

Mmoja ya wale walionukuliwa anasema kuwa bwana Kislyak alizungumza na Sessions kuhusu maswala muhimu ya kampeni ikiwemo msimamo wa Trump kuhusu sera muhimu za Urusi.

Wakati alipothibitishwa mapema mwaka huu, bwana Sessions alisema kuwa hajawasiliana na Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wakati ilipobainika aliwasiliana alisema kuwa swala la kampeni halikuangaziwa katika mkutano huo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...