Leo tarehe 23/8/2017 baadhi vijana wa JUVICUF chini ya kamati ya vyuo vikui walifika nyumbani kwa lengo la kumjuilia hali mzee wetu, MACHANO KHAMIS na kubadilishana naye mawazo.
Mzee machano ni miongoni mwa waasisi wa CHAMA CHA WANANCHI-CUF ambae kwa sasa anasumbuliwa na maradhi ya uzeeni. Huenda wengi wa vijana hata hawamfahamu mzee huyu.
Miongoni mwa aliotusimulia na kutueleza kwa kina ni historia ya mapambano ya kutafuta haki kwa kila Mtanzania.
Akisimulia wakati walipofukuzwa kutoka katika CCM alisema.
"...kabla hatujafukuzwa, akina Salim Ahmed Salim walimwambia Nyerere, ukiwafukuza hawa CCM utakuwa kushaiuwa Zanzibar. Na ni kweli CCM tulizika kabisa."
Tulimuliza kama lau akipewa nafasi ya kupendekeza ni nani awe mrithi Maalim alisema. "NI NYINYI VIJANA. Sisi shida yetu ni mtu yeyote atakaekuwa tayari kupigania maslahi ya wananchi wa Zanzibar na Bara. Kila mtu apate haki yake kwa usawa kabisa"
Alipoulizwa ni wasifu gani haswa anaojipambanua Maalim Seif anaoufahamu. Mzee machano alisema.
*Maalim ana tabia moja.*
*Hana unafiki moyoni mwake.*
*Haongopi katika maneno yake.*
*Haanguki katika mipango yake.*
*Akikuahidi basi atatekeleza*
Na alipoulizwa kama ni lini alikutana na Maalim. Alisema kuwa ni hivi karibuni tu. Maalim huwa anakuja hapa na kunisalimia. Na hajawahi kunitupa hata kidogo.
Kuhusu suala la ukombozi wa Zanzibar alisema.
*Zanzibar itakomboka leo hii kabla ya kesho. Hatuwezi kuelekea 2020 kama Zanzibar haipo mikononi kwetu. Maalim atakuwa Rais kabla ya 2020. Nina hakika na matumaini makubwa*
Tulikuwa na mengi sana tuliojifunza. Ila kubwa ni maneno yake ya busara kwetu vijana.
*Nakuhusieni kutokuyumbishwa. Nendeni mkawakomboe vijana wenzenu waliofungwa mawazo. Na PENDENI NCHI YENU KWANZA KISHA NDIO MUJIPENDE WENYEWE*
Namuombea kwa Allah ampe afya njema ili awe nasi siku ya jua jipya kichomoza. Ampe hatima njema pale atapomuhitaji mja wake.
MOH'D RAJAB.
Mkuu wa idara ya vyuo vikuu,
JUVI-CUF TAIFA.