» » KAMA VIJANA TUNGETAMBUA MAANA HARISI YA NENO NAKUPENDA

HUENDA TUNGEKUWA MAKINI NA VINYWA VYETU KATIKA KULITAMKA!!!,

Binti toka Kupevuka kwako  umeambiwa na wangapi kuhusu kupendwa??Na wangapi bado wapo nawe hata Leo????Kwanini nataka kulizungumzia hili,nimeona tatizo kubwa kwa wadada.Wengi wanashindwa na kutatanishwa kumwelewa yupi ni mwanaume sahihi na yupi Mwongo.

Hebu fikiria kijana aliyekutoa usichana wako alikuahidi mengi na alidai ANAKUPENDA yupo wapi Leo???Baada ya huyo wa kwanza kukuharibia usichana wako na kutokomea ni kana kwamba amefungua mwanya kwa matapeli wengine wa mapenzi kukuandama na kila mmoja anadai kukupenda,ukimkubalia huyu baada ya mda anakutelekeza.Na kila mwanaume anakuja na njia ya kusema anakupenda na anampango wa kukuoa.Kwanini ukishampa anakuona Samadi na kukukimbia???

Ni binti wachache wanaoweza kufikiria hili,ila walio wengi hurudia yale Yale .Usipo jihurumia na maisha yako wewe mwenyewe hakuna atakayekuhurumia.

NENO NAKUPENDA "" halipaswi kutamkwa ovyo ovyo au bila sababu.Hivyo binti ufahamu kabisa mwanaume anayekupenda ni mmoja tu hapa duniani.Huyo ndiye mume wako wa ndoa.

Hawa wengine ni  wa mda tu na ukikaa vibaya wataharibu hata dira yako kimaisha.

-kama wewe ni mtu wa mataizi Utashindwa kutambua ,ALIYEKUTAMANI UTASEMA AMEKUPENDA.
-Kama hutakuwa mtu wa maombi na kumtegemea Mungu utaishia kwenye mikono isiyo salama, katika mahusiano hakunaga nadharia.Fahamu kuwa  maisha ya Mahusiano bila kumtanguliza Mwenyezi Mungu hayaendi kabisa.
-Fahamu kuwa Mwanaume ALIYE KUTAMANI ATASEMA PIA ANAKUPENDA,Mwanaume aliyekutamani anatafuta jambo moja tu kutoka kwako.Akipata kibarua kimeisha.

ANAYEDAI ANAKUPENDA UNADHANI ATAAKISI HICHO ANACHOKITAMKA???

-Atakuvumilia kwa ahadi utakazo mpatia au ni mtu wa mkato???
-Atakujali kwa hali uliyonayo na wazazi wako??
-Atakuwa bega kwa bega nawe katika kipindi chote cha maisha.
-Unadhani ni kweli anaweza kuwa mashauri bora kwako ???
-Atakusaidia kufikia ndoto zako???

MWANAUME ANAWEZA KUKUPUMBAZA KWA HAYA YAFUATAYO;
-Atakupangushia chumba au nyumba akija kukutembelea utakataa??La Hasha utampa tu:
-Atakununulia vitu vya thamani simu ,nguo na kukupeleka sehemu za starehe kwa akili yako utadhani anakupenda kumbe anakupumbaza akili,ukimpa anakutelekeza:
-Atakufungulia biashara,ukishapumbazika ukampa anaangalia wengine.
MWANAUME WA MALENGO NI YULE TU ATAKAYE PATIKANA KWA MAOMBI YA IMANI.TUSIFARIJIANE KAMA HUTAKUWA MTU WA MAOMBI MAHUSINO YANAWEZA KUBAKIA KUWA CHANGAMOTO KWAKO .

WANADAMU TUNABADILIKA BADILIKA,UNAVYOMWONA LEO SIVYO UTAVYOMWONA KESHO.KIMTAZAMO NA KIITIKADI NA KIUMBO ANAWEZA KUBADILIKA.

UZURI WAKO UTAKULETEA WANAUME WENGI ILA WASIO NA MALENGO NAWE.

GOD IS LOVE.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...