» » *SIFA ZA MTU MASKINI...!*

(1). HUWAZA KUSHINDWA.

Akili yake inaona matatizo tu, haioni fursa na uwezekano wa kufanikiwa.(MARKO 9:23

(2). HUZUNGUMZA KUSHINDWA.

Hujaa masononeko na lawama, siku zote huzungumzia ugumu tu maisha.(MITHALI 23:7a)

(3). ANA VISINGIZIO VINGI.

Hupenda kutupia lawama kwa watu wengine kutokana na hali yake aliyonayo. Anaweza akawalaumu wazazi wake kwanini hawakumsomesha,au hawakumpatia mtaji wa kuanza biashara, kusema ndugu zake hawamsaidii n. k. (WAFILIPI 2:14)

(4). MVIVU.

Uvivu na umaskini ni mapacha wanaofanana. Maskini hapendi kujishughulisha yeye anapenda vitu vingi afanyiwe au akute vimefanywa na yeye kazi yake ni kuvitumia tu.Wanapenda kulala muda mwingi (MITHALI 10:4)

(5). HUWA NA MATUMIZI MABAYA YA PESA.

Kushindwa kuwa na maamuzi sahihi ya pesa ni njia ya kuelekea kwenye umaskini.Mtu wa namna hii akipata pesa yupo tayari kabati lake kulijaza nguo mpya kuliko kuiwekeza hiyo pesa kwenye biashara hata kama ni ndogo (MITHALI 21:5)

(6). HUAMINI MAFANIKIO YAPO KWA MTU MWINGINE.

Hawezi kujitegemea, anaamini bila fulan kumsaidia maisha hayawezi kwenda, Hata kama hakuna ulazima wa kumtegemea mtu /watu.(MITHALI 17:5)

(7). HAWEKEZI.

Hutumia pesa yote inayopita mikononi mwake kwa kula na kuvaa. Haweki akiba wala Hawekezi. Ndio wale wanaoamini msemo usemao,"ponda mali kufa kwaja " wanajiita wazee wa kula bata.(MITHALI 21:20a ;13:11)

(8). HAPENDI KUANZIA CHINI.

Huchagua kazi za kufanya, hataki kuanzia chini ili apande kimaisha taratibu. Anaamini anaweza kujenga ghorofa bila kuanza na kibanda.Anaona kuanza biashara yenye mtaji mdogo ni kijidharirisha (ISAYA 51:2)

(9). HUWASEMA VIBAYA WALE WALIOFANIKIWA.

Huamini wale waliofanikiwa walibahatika tu, walisaidiwa au kurithi mali, wakati mwingine huwahusisha kuwa walifanikiwa kwa kutumia nguvu za giza /kishirikina.(MITHALI 10:31-32)

(10). HAKUBALI KUJIFUNZA.

Hataki kuwa tayar kujifunza kwa waliofanikiwa. Badala ya kujenga nao urafiki, yeye anajenga uadui. Badala ya kuomba mbinu zitakazo muwezesha kufanikiwa, yeye huomba pesa kwa waliofanikiwa. Hapendi kujifunza, Mvivu wa kusikia maarifa.(MITHALI 1:22)
*........KAMA WEWE UPO HIVYO BADILIKA.............
HUU NI WAKATI WA KUWAFUNDISHA WATU KWELI ILI WAPATE KUFANIKIWA KIMWILI NA KIROHO PIA WASIKAE NA KUSUBIRI MIUJIZA YA KUPOKEA GARI, KUPOKEA NYUMBA e.t.c.........................................*
Umaskini sio hali ya kukosa mali na kuwa na hali duni, umasikini ni mtazamo usioweza kuzalisha, usiowaza kufanikiwa, usiotaka kujituma.Ebu pokea hili wazo la utajiri upate kufanikiwa, nawewe uliyefanikiwa acha kuwaza kimaskini.
Yupo maskini mwenye mawazo ya utajiri, na yupo tajiri mwenye mawazo ya kimaskini tumia utajiri wako kwa ajiri ya kazi ya BWANA.
" Change your MIND, before you change your LIFE ".
*YOU ARE WHO YOU ARE BECAUSE OF YOUR MIND*..!

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...