» » Seneta John McCain apatikana na saratani ya ubongo

Haki miliki ya pichaAFPImage captionAliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani John McCain apatikana na saratani ya ubongo

Seneta wa chama cha Republican John McCain amepatikana na saratani ya ubongo na anatafuta matibabu kulingana na duru za offisi yake.

Matibabu hayo huenda yakashirikisha matumizi ya dawa ama mionzi kulingana na daktari wake.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80 yuko katika hali nzuri akiendelea kupata afueni nyumbani.

Uvumbe huo ulipatikana wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la kushoto.

Viongozi wa Republican wazidi "kumtema" Donald TrumpTrump awaidhinisha mahasimu wake wa RepublicanKutana na wale wanaotarajiwa kuwa mawaziri wa TrumpSababu zilizosababisha Trump Kushinda

McCain ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam pia alitumikia miaka mitano jela.

Seneta huyo aliyehudumu kwa mihula sita na kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican 2008 alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona siku ya Ijumaa.

Uchunguzi wa tishu ulibaini kwamba uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma ulisababisha damu hiyo kuganda kulingana na taarifa ya kliniki hiyo ya Mayo.

Madaktari wa Seneta huyo wanasema kuwa anaendelea kupona kutoka kwa upasuaji huo na afya yake iko shwari, iliongezea.

Matibabu yake yatashirikisha utumiaji wa dawa na mionzi.

Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa ubongo na huongezeka kutokana na umri wa mtu ukiwaathiri wanaume wengi zaidi ya wanawake.

Bwana McCain ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya sineti kuhusu hudumu za jeshi alikuwa katika hali nzuri huku akiendelea kupona nyumbani na familia yake, afisi yake ilisema.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...