» » Sasa Marekani na K. Kusini zaonya kuishambulia Korea Kaskazini


Image captionRais Trump na mwenmzake wa Korea Kusini Jae-Moon. Mataifa yao yameonya kuishambulia Korea Kaskazini

Marekani na Korea kusini zimeionya kwa pamoja Korea Kaskazini kwamba huenda kukazuka vita kufuatia hatua ya taifa hilo kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu siku ya Jumanne.

Maafisa wawili wakuu wa mataifa hayo mawili walio na makao yao Korea Kusini wamesema kuwa kujizuia ni chaguo lao na kwamba hatua hiyo inaweza kubadilika wakati wowote.

Wamesema kuwa itakuwa ''makosa makubwa'' kutofikiria kuchukua hatua kali.

Onyo hilo linajiri wakati ambapo mataifa hayo mawili yamefanya zoezi la pamoja la kijeshi la makombora ya masafa marefu.

Image captionPresident kim Jong Un

Kituo cha habari cha Korea Kaskazini kilimnukuu kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un akisema kuwa jaribio hilo la kombora la masafa marefu ni zawadi kwa Wamarekani wakati was siku yao ya uhuru .

Mapema, waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson aliionya Pyongyang kwamba inaendeleza vitisho dhidi ya Marekani na dunia nzima kwa jumla.

Download Apps Yetu Gsn News

Au tutafte kwa 0769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...