» » Mwakyembe Leo Kaongea na Waandishi wa Habari Baada ya Msiba wa Mkewe 


Leo Jumatano ya July 26 ikiwa ni siku 11 zimepita toka utokee msimba wa mke wa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Dr Harrison Mwakyembe, leo ameongea na vyombo vya habari nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam.

Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan.

Dk Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.
  
 ==>Ulizisoma hizi??
    1.Serikali yatangaza nafasi 150 za kazi za Udereva wizara mbalimbali. 

    2.Nafai 48 za Kazi Toka Tanzania Public Service College (TPSC)

Mbali na hao, Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela Mkoani Mbeya, amewashukuru viongozi wote wa dini akiwamo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zuberi na maaskofu.

"Wanafamilia tutakumbuka moyo adhimu na upendo na ushirikiano tulioupata kutoka Katibu Mkuu wa wizara hii Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Mwisho kabisa Wanakyela kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki kigumu," amesema Dk Mwakyembe.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles