» » Mkuu wa wilaya ataka mbunge wa upinzani akamatwe Tanzania



Maafisa wa serikali nchini Tanzania wameamuru kukamatwa na kuzuiliwa kwa mbunge wa chama cha upinzani kwa tuhuma za kumtusi Rais John Magufuli, taarifa zinasema.

Polisi wametakiwa kumkamata na kumzuilia Halima Mdee, ambaye ni mbunge wa chama cha Chadema, mjini Dar es Salaam akisubiri kufunguliwa mashtaka ya uhalifu.



Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIAImage captionRais wa Tanzania John Magufuli

Agizo la kumkamata limetolewa na mkuu wa wilaya Kinondoni Ali Hapi.

"Anafaa kuhojiwa na kupelekwa kortini kutoa ufafanuzi kuhusu matusi aliyotoa dhidi ya rais wetu," Bw Hapi aliambia wanahabari.

Magufuli ayaonya magazeti TanzaniaMagufuli: Wananchi wanahitaji maendeleoMatamshi ya Magufuli yawakasirisha wanawake Tanzania

Taarifa zinasema Bw Hapi alisema mbunge huyo alinena maneno ya matusi wakati wa mkutano wa chama chake Jumatatu asubuhi.

Mkuu huyo wa wilaya aliambia wanahabari kwamba Bi Mdee alimtaja rais kwa jina na akasema kiongozi huyo wa nchi amekuwa na tabia mbaya na kwamba ameanza kufikiria maneno yake moja kwa moja ni sheria.

Mwaka 2015, sheria ya makosa ya uhalifu wa kimitandao ilipitishwa ambayo ilifanya kumtusi rais kuwa kosa la jinai.

Kwa mujibu wa Reuters, watu zaidi ya 10, wakiwemo wanafunzi wa vyuo na mhadhiri wamekamatwa na kufikishwa kortini miezi ya karibuni kuhusiana na kumtusi rais kupitia mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp.

Sheria nchini Tanzania zinawaruhusu makamishna na wakuu wa wilaya kumzuilia mtu yeyote kwa saa 48 iwapo ataamini kwamba mtu huyo anaweza kuvuruga amani.

Rais Magufuli aliwatahadharisha viongozi wa upinzani Jumapili dhidi ya kutoa matamshi ya kiholela na kuwaamuru maafisa wachukue hatua dhidi ya kiongozi yeyote yule wa upinzani anayechochea vurugu, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Taarifa kutoka Ikulu ilisema Rais alipokuwa anaweka jiwe la msingi na kuzindua kazi za mradi wa ujenzi, ukarabati na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam aliwataka Watanzania kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupigania maslahi ya nchi.

Kiongozi huyo wa nchi alionya dhidi ya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakibeza juhudi hizo pamoja na juhudi za kukabiliana na wahalifu ambao wanawaua raia wasio na hatia pamoja na askari polisi.

"Wajifunze kufunga midomo yao wakati Serikali inafanya kazi yake, na kwa ujumbe huu nataka Watanzania waelewe kuwa tuna mambo makubwa katika nchi hii tunayoshughulika nayo, na ndio maana wakati mwingine unakuta ni mzahamzaha tu, unakuta wakati mwingine mnashughulikia rasilimali za Watanzania zinazoibiwa, mtu mwingine anapinga hadharani" alisema Rais Magufuli.

Halima Mdee amewahi kukamatwa na kuzuiliwa Tanzania mwaka 2014 akituhumiwa kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku..

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...