Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais wa Ukrain Petro Poroshenko (wa pili kulia) akikutana na maafisa huko Donetsk mwezi Juni
Mjumbe mpya wa Marekani nchini Ukrian anasema kuwa Marekani inatathmini ikiwa itatuma silaha kusaidia wale wanaopigana na waasi wanoungwa mkono na Urusi.
Kurt Volker aliiambia BBC kuwa kuihami serikali ya Ukrain itabadilisha msimamo wa Urusi.
Alisema hafikirii kuwa hatua hiyo itakuwa ni uchokozi.
Ukrain: Urusi ilihusika na udukuzi wa mitandaoMapigano mapya mashariki mwa UkrainUkrain yakiuka onyo la Urusi na kufanya mazoezi ya kijeshi
Wiki iliyopita wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Marekani ilizitaka pande zote mbili kusitisha mapigano mashariki mwa Ukrain.
"Silaha za kujilinda, zile ambazo zitaisaidia ukrain kujilinda na kuharibu vifaru kwa mafano, ambazo zitaizuia Urusi kuitisha Ukrain," bwana Volker aliiambia BBC.
Image captionEneo linalokaliwa na waasi nchini Ukrain
Alisema kuwa mafanikio ya kuwepo amani mashariki mwa Ukrain yanahitaji kile alichokitaja mchakato wa mazungumzo na Urusi.
Bwana Volker na mjumbe wa zamani wa Marekani kwenye Nato na aliteuliwa kwenye wadhifa huo mpya mwezi huu.
Trump aitaka Urusi kuwacha kuivuruga UkrainUrusi kuvuruga matangazo ya radio kutoka Ukrain kwenda Crimea
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wameuawa tangu mzozo wa Mashariki mwa Ukrain ushuke mwezi Aprili mwaka 2014 mara baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea.
Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni 1.6 kuhama makwao.
No comments:
Post a Comment