» » Acacia yakataa kuilipa Tanzania deni la $180b


Haki miliki ya pichaACACIA MININGImage captionLori linalotumika katika ubebai wa madini

Serikali ya Tanzania imesema kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu yenye makao yake nchini Uingereza Acacia inadaiwa na walipa kodi dola bilioni 180 ,kama malipo ya adhabu na riba, kulingana na taarifa ya kampuni hiyo.

Takwimu hiyo ni kulingana na ufichuzi uliofanywa na tume mbili za rais kuhusu sekta ya uchimbaji madini.

Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Awamy deni hilo linalodaiwa Acacia linasimia mapato yaliopatikana ambayo hayakutajwa kutoka kwa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi katika kipindi cha mwaka 2000 na 2017.

Mambo muhimu kuhusu sakata ya madini TanzaniaBunge la Tanzania lapitisha sheria za madiniRipoti ya Madini:Rais Magufuli amshauri Waziri ajiuzulu

Ikijibu, Acacia imepinga madai hayo na kusema kuwa inatafuta njia mbadala

Uchunguzi uliofanywa na tume hizo za rais uliishutumu Acacia kwa kufanya operesheni zake kinyume cha sheria na kushindwa kulipa inachodaiwa.

Acacia ambayo ndio kampuni kubwa inayochimba madini nchini humo ,imesisitiza kuwa imekuwa ikitangaza mapato yake.

Katika mkutano wa hadhara siku ya Ijumaa rais John Magufuli alitishia kufunga migodi yote ya dhahabu nchini humo iwapo kampuni za kuchimba madini zitachelewa kufanya mazungumzo na serikali yake yanayolenga kutatua madai ya ukwepaji kodi.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...