» » Uchaguzi Kenya: Matokeo ya urais kutangazwa rasmi kwenye maeneo bunge

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya Bw. Chebukati anasema tume hiyo imejiandaa vyema kwa zoezi la uchaguzi

Mahakama ya Rufaa imeamua matokeo rasmi ya kura za urais yatatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi vituo vya kuhesabu kura kwenye maeneo bunge.

Uchaguzi wa Kenya utafanyika tarehe nane mwezi Agosti mwaka huu ambapo Rais Uhuru Kenyatta atang'ang'ana kuhifadhi wadhifa wake dhidi ya mpinzani wake wa jadi Raila Odinga.

Uchaguzi wa Kenya: Maswali muhimu na majibu

Uamuzi huo wa majaji watano wa Mahakama ya Rufaa umeonekana kama ushindi mkubwa kwa muungano wa upinzani.

Jopo la majaji watanao limesema kwamba mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC hana mamlaka kisheria ya kuhakiki na kutangaza matokeo ya urais.

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionWakenya wakiwa kwenye foleni za kupiga kura

Msimamo wa tume ya uchaguzi, ni kwamba lazima maafisa wake wahakiki matokeo yote kutoka maeneo bunge katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura, na kwamba wana uwezo wa kubadilisha matokeo hayo.

Serikali ilikuwa inaunga mkono msimamo huo, japo upinzani ulipinga.

Wagombea wanane watakaowania urais Kenya Agosti

Kwa muda mrefu upinzani umekuwa ukieleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa muungano tawala kushirikiana na tume ya uchaguzi kuhujumu matokeo ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi imekana madai hayo.

Uchaguzi wa agosti 8, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa baina ya rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga.

Mahakama hiyo pia ilisema mahakama ya juu ina uwezo wa kisheria wa kutatua mizozo inayotokana na uchaguzi wa urais.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...