SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 35.
Tulipoishia, Kisha kulikuwa na barua. Wakati natafakari Kuichukua barua ile mara nikasikia mlio wa risasi ukiwa umetokea walipo baba na mama. Nilishtuka nikageuka na kukimbilia mara nikaona_______Songa nayo........ Baba yangu akigaragara chini. Nikamkimbilia na kumwamgalia nikaona amepigwa risasi maeneo ya bega. Nikainuka na kuangalia kama nitamwona mtu sikumwona na nilipopepesa macho nikaona kimya kimetanda. Mama yangu alikuwa kaanguka chini nadhani alikuwa kazimia. Kwakuwa tayari nilikuwa na uzoefu nilijuwa kwa maeneo ambayo baba kajeruhiwa si rahisi kuaga dunia.
Nikaamua kuanza kushughulika na mama mpaka alipozinduka. Ndipo nikakimbilia gari langu na huko nikakuta mapya tena. Bunduki zile sikuziona wala zile risasi. Sikulijali hilo nikaandaa mazingira nikampakia baba tayari kumuwahisha hospitalini. Ilikuwa ni mbali sana kutokea kijijini lakini nilijitahidi kukimbia na gari ili walau kuokoa maisha ya baba. Nilikuwa na hasira haswaa kwani niliona hali imekuwa tete. Nani ananifuata mpaka kijijini ama kweli. Je ni nani amewaambia mimi nimetoka? Hapo nikaanza kumtilia mashaka Oscar kwani hakuna aliyejuwa nimerudi uraiani zaidi ya Oscar na Yule aliyenisaidia kutoroka. Hao tuu ndio nilikuwa na mashaka nao.
Nikaamua kutuliza kichwa kisha yeyote atakayegundulika kunigeuka ni haki yangu. Baada ya mwendo mrefu tulifika hospitalini lakini wakati tunamtoa babangu kwenye gari. Tukiwa mimi na mama yangu mara kuna mlio wa risasi ukasikika tena na huu ulimfanya mzee wangu kupigwa risasi ya pili mguuni. Gadhabu ikanivamia nikamwachia mzee na kuangalia kama nitaona kitu lakini sikuona. Nilipepesa macho huku na huko lakini sikuona chochote. Hali hii ilinitisha sana. Nikaamua kurudi nimuwahishe baba ndani ya hospitali kisha niangalie nifanye nini.
Niliumia sana kwakweli lakini sikuwa na jinsi. Baada ya baba kumkabidhi mikononi mwa madaktari nikatoka nje na kumpigia simu Oscar nikamwuliza maswali mengi sana. Lengo nilikuwa nahitaji kujua kama kuna ushirikiano wowote baina yake na majambazi. Alikana kwa nguvu zote kisha nikamwuliza kwani ni nani anajua mi niko kijijini zaidi yako? Akajibu kwakweli Bro yuu umenisaidia mambo mengi nikikuwa mtu wa mtaani mvuta bangi nisiye na mbele wala nyuma. Nguo zangu zilijaa vilaka mpaka vinaulizana mwenzangunulikuja lini? Miguu yangu ilikuwa mithili ya gamba la kobe! Leo hii napendeza nimenawiri kisha nikusaliti kaka Yuu? Nitakuwa mpumbavu na nisiye na hekima. Siwezi kaka yangu siwezi nakuheshimu niko tayari kuku........... Ku.... Mara akawa kama anashindwa kuongea.
Mara sauti ikabadilika Nikasikia Zabroni Makweka niko nyumbani kwako. Najua umetoka jela umerudi kulipa kisasi. Nina taarifa zako. Sasa sikia hicho kilichotokea kwa babako ni onyo. Bora umetoka jela lakini ungeamua kwenda kulima ungekua uamuzi wa busara kuliko kupambana na serikali. Nilipigwa na butwaa mara kuna mlio wa risasi na kelele zikasikika aaaaaaahhhhhh!!!! Na simu ikakatika nilipoipiga tena ilikuwa haipatikani. Niliingiwa na woga nakuhisi huenda Oscar kauawa. Nilikuw niko mbali na jiji la Dar es salaam ningefanya nini unadhani? Sikuwa na mtu wa kumpigia japo simu kwani mambo yangu yangeharibika. Pia ikumbukwe nilikuwa nimetoroka jela. Hivyo kupiga simu ovyo ingefanya kila mtu kujua kuwa niko wapi.
Nikaamua nirudi wodini kumwangalia baba yangu na kama hali yake iko vizuri asi nirudi mara moja jijini Dar es salaam. Na wakati naingia nilimwona mama analia nikamtuliza kiasi akatulia nikamweleza kuwa Dar es salaam kuna tatizo limetokea vipi hali ya baba? Akajibu hali ya baba siyo nzuri sana ila maweza kwenda yeye atamwangalia kwa ukaribu kikubwa nilipie kabisa. Nikaenda kumwona baba alikuwa kalala usingizi. Niliumia sana lakini ilinilazimu kuondoka.
Nilienda sehemu ya malipo na kulipia kila kitu.kisha nikarudi kwa mama na kumwachia pesa ya kutosha matumizi na pia kuwasukuma kwa kipindi chote ambacho sitakuwepo. Zilikua ni pesa nyingi sana kwakweli. Mama alishukuru sana na kunipa baraka za kulipa kisasi. Sasa huo mziki unaoenda kuchezwa huko tena una baraka. Nadhani mmasai akiingia na rungu na sime atakuwa kapotea. Nilitoka hospitalini mda uleule. Sikutaka kupoteza mda.
Niliendesha gari kama mtu nisiye na akili timamu. Nilifika Dar es salaamu usiku sana. Sikutaka kuingia na gari nyumbani kwangu. Niliipaki mbali kabsa na Nyumbani kisha taratibu kwa kujihami nikaanza kusogea nyumbani. Nikweli nilichoka na safari lakini ilinilazimu kwani mambo yalikuwa magumu. Nilifika getini na kuhisi kuna utofauti mkubwa na palivyozoeleka. Palikuwa panaonekana si salama sana hivyo ilinibidi nijihadhari. Nikasonga mbele na kukaribia mlango nikaufungua na kukuta sebuleni damu zimetapakaa.
Nilishtuka sana. Zaidi kilichonishitua ni vile nilivoona taa zinawaka. Nikaangalia vizuri sebuleni sikuona kitu zaidi ya Damu. Nikaamua kuingia chumbani. Huku ndiko ilikuwa majanga. Kwani wakati naondoka chumba niliacha kisafi na kina marashi safi. Lakini wakati huu narudi hali ilikuwa tofauti. Wakati nasukuma mlango kuna hewa chafu, ya uvundo na uozo wa mnyama mfu ilinisukuma kurudi nyuma. Ilikuwa hewa nzito na isiyovumilika. Ilinisukuma mpaka nikajikuta niko sebuleni. Lakini nikajipa moyo ya kuwa ngoja niingie nijue kuna nini?
Wakati nimejilazimisha kuingia kwenye ukungu wa harufu. Nilijikuta napaliwa na kukohoa mara kadhaa. Nikapepesa macho huku na kule ndipo sikuamini ninachokiona mbele yangu. Ilikuwa ni maiti ya yule meneja wa benki. Niliyemuua na kuiba fedha. Swali ni je ile maiti imefikaje kwangu? Na waliipulizia madawa ili ioze haraka inuke na watu waje kukagua mwangu. Hivi ndivyo ingefahamika kuwa Yuu katoroka Jela na kukamatwa upya. Walikuwa wana mipango ya mbali sana hawa watu. Niliwaza na kujiuliza nifanye nini? Kumbuka maiti ilikuwa inatoa harufu sana hivyo hali ile ingelifanya watu kuja kwangu. Nikiwa natafakari mara mlango wangu ukagongwa ngo! Ngo! Ngo!_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________ __________Je ni nani alikuwa anagonga? Usikose sehemu ya 36. Kwa kolote nichek kwa mawasiliano ayo ya juuu.nawapenda sana
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 35.
Download Apps ya Gsn News
Au nambie what's app kwa 0769436440 nikutumie Link
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment