» » Mataifa 4 ya kiarabu yaipa Qatar masharti 13 kuafikia la sivyo itengwe

Haki miliki ya pichaAFPImage captionSaudia imefunga mpaka wake wa ardhini kati yake na Qatar

Mataifa manne ya kiarabu yameitumia Qatar masharti 13 ambayo ni sharti iafikie iwapo inataka kuondolewa vikwazo kulingana na vyombo vya habari.

Saudia, Misri, UAE na Bahrain zinataka taifa hilo kufunga kitu chake cha habari cha Aljazeera.

Pia wanaitaka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran na kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.

Madhara yatakayoletwa na kuitenga QatarQatar yaapa kutosalimu amri UarabuniIndia kuwasafirisha raia wake kutoka QatarMataifa ya Kiarabu yajitenga na Qatar

Qatar imekana kufadhili magaidi hatua inayosababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Taifa hilo limekabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa kipindi cha wiki mbili ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kati ya mataifa hayo ya Ghuba kwa miongo kadhaa.

Image captionRamani ya majirani wa taifa la Qatar

Orodha hiyo ilitangazwa baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kuwaambia majirani wa Qatar ''kuweka mahitaji yao na kuchukua hatua''.

Waandishi wanasema kuwa Marekani ambayo inataka kutatua mzozo huo imekuwa na matatizo, kuhusu kipindi cha Saudia na mataifa mengine kuweka rasmi mahitaji yao.

Hakujakuwa na majibu ya moja kwa moja kutoka Qatar lakini waziri wa maswala ya kigeni Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani alisema awali kwamba Qatar haitafanya majadiliano yoyote hadi pale vikwazo hivyo vitakapoondolewa.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...