» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 35 Na 36


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 35.
Tulipoishia, Kisha kulikuwa na barua. Wakati natafakari Kuichukua barua ile mara nikasikia mlio wa risasi ukiwa umetokea walipo baba na mama. Nilishtuka nikageuka na kukimbilia mara nikaona_______Songa nayo........ Baba yangu akigaragara chini. Nikamkimbilia na kumwamgalia nikaona amepigwa risasi maeneo ya bega. Nikainuka na kuangalia kama nitamwona mtu sikumwona na nilipopepesa macho nikaona kimya kimetanda. Mama yangu alikuwa kaanguka chini nadhani alikuwa kazimia. Kwakuwa tayari nilikuwa na uzoefu nilijuwa kwa maeneo ambayo baba kajeruhiwa si rahisi kuaga dunia.
Nikaamua kuanza kushughulika na mama mpaka alipozinduka. Ndipo nikakimbilia gari langu na huko nikakuta mapya tena. Bunduki zile sikuziona wala zile risasi. Sikulijali hilo nikaandaa mazingira nikampakia baba tayari kumuwahisha hospitalini. Ilikuwa ni mbali sana kutokea kijijini lakini nilijitahidi kukimbia na gari ili walau kuokoa maisha ya baba. Nilikuwa na hasira haswaa kwani niliona hali imekuwa tete. Nani ananifuata mpaka kijijini ama kweli. Je ni nani amewaambia mimi nimetoka? Hapo nikaanza kumtilia mashaka Oscar kwani hakuna aliyejuwa nimerudi uraiani zaidi ya Oscar na Yule aliyenisaidia kutoroka. Hao tuu ndio nilikuwa na mashaka nao.
Nikaamua kutuliza kichwa kisha yeyote atakayegundulika kunigeuka ni haki yangu. Baada ya mwendo mrefu tulifika hospitalini lakini wakati tunamtoa babangu kwenye gari. Tukiwa mimi na mama yangu mara kuna mlio wa risasi ukasikika tena na huu ulimfanya mzee wangu kupigwa risasi ya pili mguuni. Gadhabu ikanivamia nikamwachia mzee na kuangalia kama nitaona kitu lakini sikuona. Nilipepesa macho huku na huko lakini sikuona chochote. Hali hii ilinitisha sana. Nikaamua kurudi nimuwahishe baba ndani ya hospitali kisha niangalie nifanye nini.
Niliumia sana kwakweli lakini sikuwa na jinsi. Baada ya baba kumkabidhi mikononi mwa madaktari nikatoka nje na kumpigia simu Oscar nikamwuliza maswali mengi sana. Lengo nilikuwa nahitaji kujua kama kuna ushirikiano wowote baina yake na majambazi. Alikana kwa nguvu zote kisha nikamwuliza kwani ni nani anajua mi niko kijijini zaidi yako? Akajibu kwakweli Bro yuu umenisaidia mambo mengi nikikuwa mtu wa mtaani mvuta bangi nisiye na mbele wala nyuma. Nguo zangu zilijaa vilaka mpaka vinaulizana mwenzangunulikuja lini? Miguu yangu ilikuwa mithili ya gamba la kobe! Leo hii napendeza nimenawiri kisha nikusaliti kaka Yuu? Nitakuwa mpumbavu na nisiye na hekima. Siwezi kaka yangu siwezi nakuheshimu niko tayari kuku........... Ku.... Mara akawa kama anashindwa kuongea.
Mara sauti ikabadilika Nikasikia Zabroni Makweka niko nyumbani kwako. Najua umetoka jela umerudi kulipa kisasi. Nina taarifa zako. Sasa sikia hicho kilichotokea kwa babako ni onyo. Bora umetoka jela lakini ungeamua kwenda kulima ungekua uamuzi wa busara kuliko kupambana na serikali. Nilipigwa na butwaa mara kuna mlio wa risasi na kelele zikasikika aaaaaaahhhhhh!!!! Na simu ikakatika nilipoipiga tena ilikuwa haipatikani. Niliingiwa na woga nakuhisi huenda Oscar kauawa. Nilikuw niko mbali na jiji la Dar es salaam ningefanya nini unadhani? Sikuwa na mtu wa kumpigia japo simu kwani mambo yangu yangeharibika. Pia ikumbukwe nilikuwa nimetoroka jela. Hivyo kupiga simu ovyo ingefanya kila mtu kujua kuwa niko wapi.
Nikaamua nirudi wodini kumwangalia baba yangu na kama hali yake iko vizuri asi nirudi mara moja jijini Dar es salaam. Na wakati naingia nilimwona mama analia nikamtuliza kiasi akatulia nikamweleza kuwa Dar es salaam kuna tatizo limetokea vipi hali ya baba? Akajibu hali ya baba siyo nzuri sana ila maweza kwenda yeye atamwangalia kwa ukaribu kikubwa nilipie kabisa. Nikaenda kumwona baba alikuwa kalala usingizi. Niliumia sana lakini ilinilazimu kuondoka.
Nilienda sehemu ya malipo na kulipia kila kitu.kisha nikarudi kwa mama na kumwachia pesa ya kutosha matumizi na pia kuwasukuma kwa kipindi chote ambacho sitakuwepo. Zilikua ni pesa nyingi sana kwakweli. Mama alishukuru sana na kunipa baraka za kulipa kisasi. Sasa huo mziki unaoenda kuchezwa huko tena una baraka. Nadhani mmasai akiingia na rungu na sime atakuwa kapotea. Nilitoka hospitalini mda uleule. Sikutaka kupoteza mda.
Niliendesha gari kama mtu nisiye na akili timamu. Nilifika Dar es salaamu usiku sana. Sikutaka kuingia na gari nyumbani kwangu. Niliipaki mbali kabsa na Nyumbani kisha taratibu kwa kujihami nikaanza kusogea nyumbani. Nikweli nilichoka na safari lakini ilinilazimu kwani mambo yalikuwa magumu. Nilifika getini na kuhisi kuna utofauti mkubwa na palivyozoeleka. Palikuwa panaonekana si salama sana hivyo ilinibidi nijihadhari. Nikasonga mbele na kukaribia mlango nikaufungua na kukuta sebuleni damu zimetapakaa.
Nilishtuka sana. Zaidi kilichonishitua ni vile nilivoona taa zinawaka. Nikaangalia vizuri sebuleni sikuona kitu zaidi ya Damu. Nikaamua kuingia chumbani. Huku ndiko ilikuwa majanga. Kwani wakati naondoka chumba niliacha kisafi na kina marashi safi. Lakini wakati huu narudi hali ilikuwa tofauti. Wakati nasukuma mlango kuna hewa chafu, ya uvundo na uozo wa mnyama mfu ilinisukuma kurudi nyuma. Ilikuwa hewa nzito na isiyovumilika. Ilinisukuma mpaka nikajikuta niko sebuleni. Lakini nikajipa moyo ya kuwa ngoja niingie nijue kuna nini?
Wakati nimejilazimisha kuingia kwenye ukungu wa harufu. Nilijikuta napaliwa na kukohoa mara kadhaa. Nikapepesa macho huku na kule ndipo sikuamini ninachokiona mbele yangu. Ilikuwa ni maiti ya yule meneja wa benki. Niliyemuua na kuiba fedha. Swali ni je ile maiti imefikaje kwangu? Na waliipulizia madawa ili ioze haraka inuke na watu waje kukagua mwangu. Hivi ndivyo ingefahamika kuwa Yuu katoroka Jela na kukamatwa upya. Walikuwa wana mipango ya mbali sana hawa watu. Niliwaza na kujiuliza nifanye nini? Kumbuka maiti ilikuwa inatoa harufu sana hivyo hali ile ingelifanya watu kuja kwangu. Nikiwa natafakari mara mlango wangu ukagongwa ngo! Ngo! Ngo!_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________ __________Je ni nani alikuwa anagonga? Usikose sehemu ya 36. Kwa kolote nichek kwa mawasiliano ayo ya juuu.nawapenda sana

SEHEMU YA 36.
Tulipoishia, Walikuwa wana mipango ya mbali sana hawa watu. Niliwaza na kujiuliza nifanye nini? Kumbuka maiti ilikuwa inatoa harufu sana hivyo hali ile ingelifanya watu kuja kwangu. Nikiwa natafakari mara mlango wangu ukagongwa ngo! Ngo! Ngo!______Woga ukaniingia taratibu nikahisi kumalizwa kiakili. Nikaanza kutetemeka nikijiuliza huyo ni nani au mwisho wangu umefika? Lakini kwa mbali nikasikia sauti ya marehemu mke wangu ikisema. Yuu najua unaweza kuwamaliza. Ua wote, te.. tee... Ikaishia kwa mwangwi ndipo roho ya ujasiri na kujiamini ikanivaa. Nikajikuta napata nguvu mpya. Taratibu nikawasogea mlangoni na kuufungua mlango. Chaa ajabu sikuona kitu. Nilitoka nje na kuangalia kwa makini lakini sikuona kitu. Nikajiuliza nani kagonga? Hawa akina Zabroni mbona wana nitesa hivi?
Hivi ni akina nani haswaa? Mbona kila nifanyalo wanajua? Au ni majini hawa? Wamenifunga jela hawakuridhika? Wameniiulia mke na wanangu wawili tena vifo vya aibu! Tazama wameua kila nilichokitegemea. Wanataka kumuua baba yangu hawa ni akina nani? Kila hatua ninayopiga wanaijua kwanini? Hapana! Hapana! Lazima kuna namna haiwezekani ikawa hivi. Lazima kuna kitu. Hayo yalikuwa mawazo yangu kichwani. Kisha nikarudi ndani na kuamua jambo moja tuu kuuzika ule mwili wa meneja wa benki.
Nilikuwa sasa nimevaa roho ya unyama. Nikatoka nje nikachimba shimo na kurudi ndani nikauchukua ule mwili na kuufukia nje ya uwanja wangu. Kisha nikaamua jambo moja kurudi jela kwa njia za panya nikamwangalie yule mjinga kama yupo aseme vizuri. Wakati huo wote sijui Oscar yuko wapi kila nilipopiga simu yake ilikuwa haipatikani. Basi nikavaa nguo zangu zile za jela kwani nilizificha ndani. Kisha nje nikavaa nguo za kawaida na kuondoka mle ndani. Kulikuwa tayari kuna pambazuka nilifanikiwa kufika pale kwenye ule mfuniko kwa bahati nzuri hapakuwa na watu. Nilivua nguo za nje nikazitia kwenye mfuko wa rambo kisha nikazificha sehemu.
Nikafungua mfuniko na kuanza kuzama mpaka chini. Nilipita kwenye lile bomba lenye naji yatokayo chooni yaani yanasafirisha mavi ya wafungwa. Sikujali hilo kwani lengo langu ilikuwa kukamilisha mipango yangu. Maishani mwangu niliishi nikiamini kitu kimoja tuu. "HAKUNA AWEZAYE KURUDISHA SIKU NYUMA NA KUBADILI MWANZO MBAYA. LAKINI KILA MTU ANA NAFASI YA KUTENGENEZA MWISHO MZURI". Ningeliogopaje kinyesi wakati nataka mwisho mzuri. Nilijikaza na kujiogeza hatimaye nikaingia jela. Mungu wa ajabu wakati nafika tuu ilikuwa ni ukaguzi wa wafungwa hivo na mimi nikaonekana nikitokea chooni hakuna alinishtukia.
Nilifika nikakaguliwa vizuri. Ila nikaulizwa mbona suruali yako mbichi kama vile ulikuwa unatembea kwenye maji? Nikajibu nilikuwa chooni nikaona kuchafu nikaamua kufanya usafi. Basi hawakuendelea kunihoji. Lakini kuna wafungwa kadhaa walionyesha kugundua ya kuwa mimi nilitoroka jela siku chachw zilizopita kwani walikuwa wakilala karibu na mimi. Sikuwajali mimi niliangalia kilichonipeleka. Ndipo mpaka ukaguzi unaisha Yule mwanaharamu sikumwona.
Nilijaribu kutafuta karibu kila kundi la wafungwa lakini sikumwona. Nikajua tayari nimechezewa akili. Nikajisemea moyoni kwanini walinitoa nikapate taabu. Lakini kuna nafsi nyingine ikanisemesha moyoni hiyo ni nafasi nzuri ya kuwamaliza. Fanya utoke nikaamua kusikiliza sauti ya nafsi yangu hivyo taratibu nikaanza kurudi chooni ksha nipotee jela. Baada ya kufika nje kwa taabu sikuona tatizo nikachukua nguo zangu nikavaa kisha nikatoweka. Nilifika nyumbani kwangu na kupumzika nikitafakari yale yote. Nilimkumbuka mke wangu. Nikakumbuka nilivyolawitiwa jela. Nikakumbuka mwanangu alivyolawitiwa na kuuawa. Nikakumbuka mke wangu alivyobakwa na watu zaidi ya sita, nikakumbuka mateso ya baba kupigwa risasi bila hatia. Nikajikuta namwaga chozi chini.
Kwakuwa nilikuwa nimechoka niliamua kulala kiasi. Nilipoamka mda ulikuwa umekwenda sana nikaamua niende ufukweni mara moja japo ni mfungwa niliyetoroka jela lakini naweza kujibadili kiasi nisigundulike. Ndipo kuna kofia fulani ilikuwa na rasta nyingi, na kwakuwamimi ndevu nilikuwa sijanyoq siku nyingi nilionekana kama "rastaman" fulani. Nikatoka na kwenda fukwe za koko huko bahari ya hindi. Nilipumzika sehemu nikiwa natafakari hili na lile. Zaidi nilikuwa natafakari njia nitakazotumia kuwakamata wale wajinga. Mara simu yqngu ikaita kuangalia alikuwa ni mama yangu kijijini. Nikapokea na kusikia mama analia sana kisha akanitaarifu kwa shida ya kuwa baba yangu kafariki.
Nilijitahidi kumwuliza mama ni nini chanzo hakuweza kunambia. Nadhani ilikuwa ni kwasababu ya uchungu. Ndipo nikaamua kumpigia nesi fulani alikuwa pale hospitalini ili anipe ripoti kamili. Nesi huyu nilichukua namba zake wakati nimempeleka baba. Na nilipompigia alipokea nikamweleza ya kuwa baba yangu kafa anisaidie kunisomea ripoti ya kilichomuua ni nini? Ndipo akasema subiri nifuatilie kwa ukaribu. Baada ya mda alinipigia simu na kunambia inaonyesha marehemu alilishwa sumu kali sana. Kama si kwakuchomwa kabisa na sindano.
Nilishtuka na kumuuliza sasa sumu imetokea wapi? Nesi akajibu hilo swali mimi nashindwa kujibu njoo mwenyewe umwone daktari akueleweshe zaidi. Niligadhabika sana nikakata simu. Wakati nataka kuinuka pale nilipokuwa nimekaa. Ndipo mbele yangu nikanwona mtu ambaye anaisumbua Tanzania. Alikuwa kajishikiza kwenye Meza yangu. Moyo ulilipuka paah! Pale nilipomwona Uso kwa uso Zabroni Makweka. Hasira ikanivamia. Taratibu nikajikuta nagadhabika ile nataka kuinuka mara nimasikia mlio wa mtu akiiandaa bunduki kufyatua risasi. Mara ghafla___________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Hahahahahahaaaaa pole kwa kukukatisha utamu jamani. Tukutane kesho sehemu ya 37. Wengine eti lete sshv hahahahahahaaaa jamani. By the way Nawapenda sanaaaaaaaaaaaa..

Usisahau ku share na kudownload apps ya GSN NEWS Kama  Huna au nambie nikupe link uDownload nitumie sms kwa 0769436440

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles