Polisi nchini Ufaransa imemkamata mtu mmoja katika jiji la Paris baada ya kujaribu kuendesha gari kwa kasi mbele ya umati wa watu nje ya msikiti mmoja.
Shambulizi hilo lilitokea katika kitongoji cha Créteil na hakuna aliyejeruhiwa.
Mtu huyo hakuweza kutimiza azama yake baada ya kushindwa kuvipita vizuizi vilivyokuwepo mbele ya msikiti huo.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema mshambuliaji huyo ana asili ya Armenia.
Lengo la shambulizi hilo bado halijajulikana.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

