Ofisi ya mwanasheria mkuu nchini Venezuela imemtaka mkuu wa zamani wa jeshi la polisi kutoa maelezo juu ya matumizi ya nguzu zilizopitiliza dhidi ya mamiz ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini humo.
Ofisi hiyo imesema kuwa kuna ushahidi wa kutosha juu ya matumizi ya nguvu zilizopitiliza kwa waandamanaji.
Antonio Benavides anatarajiwa kuhojiwa siku Julai sita.

Aliondolewa madarakani wiki iliyopita, baada ya polisi aliowapa maelekezo kuonekana wakiwafyatulia risasi waandamanaji.
Zaidi ya watu 80 wameuawa katika maandamano ya miezi mitatu ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

