» » Makaburi 10 ya pamoja yagunduliwa DRC

Waliozikwa wanasemekana kuuawa na waasi

Image captionWaliozikwa wanasemekana kuuawa na waasi
Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema kwamba imepata zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa Kasai, mahali ambapo vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia.
Mwendesha mastaka wa kijeshi Generali Joseph Ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa Kamuina Nsapu ambao wamekuwa wakipiga vita majeshi ya serikali.
Mnamo wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea kila uchao katika mkoa huo, ambapo takriban watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu.
Sio mara ya kwanza kwa makaburi ya pamoja kugundulika DRC
Image captionSio mara ya kwanza kwa makaburi ya pamoja kugundulika DRC
Umoja huo aidha ulinyooshea kidole jeshi la taifa la Kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.
Hata hivyo jopo maalum la uchunguzi wa mauaji hayo iliamua kwamba hakuna uhalifu wowote wa kivitu uliyotekelezwa na kwamba hakuna mapigano yaliyotangazwa rasmi mkoani Kasai.
Inadaiwa baadhi ya wanajeshi hao walinaswa katika kanda ya video wakiwapiga risasi raia ambao hawakuwa na silaha.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles