
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, Instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 20.
Tulipoishia Wakati huo simu ilikua bado inaita. Basi kwa kua nilikua tayari kwa lolote nikainua mkono wangu na kuelekeza ilipo simu. Kisha nikaichukua huku mkono ukitetemeka sana. Wakati nataka kubonyeza kitufe cha kupokelea Ghafla______Endelea... .......Ikakatika, nadhani kwasababu iliita mda mrefu. Ikaanza kuita tena na nikaipokea huku nikiwa na mashaka. Nikasikia Peris akisema Mume wangu uko wapi? Nikamjibu niko nyumbani kuna mauaji yametokea huku. Mau......what? aliongea kwa jaziba Peris.
Hii sasa ni ''too much'' Yuu mbona wamezidi jamani. "okey" naja sasahivi nisubiri. Kwa bahati mbaya hakukata simu alijua na mimi nimeshakata. Nilibaki nasikiliza kwa mbali nikasikia kama mtu anamuuliza enheee kasemaje uyo bwege? nikasikia jibu aaah anajiliza tuu. Nikiwa nataka kusikiliza vizuri simu ikakatika. Aaah nikaanza kuhisi kweli Peris ni msaliti. Nikainuka na kuingia chumbani kupekua baadhi ya vitu vya Peris ili nione kama atakua anaviashiria vyovyote. Nilipekua sana lakini sikuona ila nikajipa moyo na kujisemea za mwizi arobaini nitambaini tuu siku ikifika.
Wakati nageuka uso kwa uso nikakutana na Peris, hali ile ilinitisha nikagundua ya kua Peris hakua mbali na pale nyumbani. Nikamwangilia hakuonyesha kushtuka sana. Nikamwonyesha kwa kidole vilipo vipande vya mwanetu akaangalia kisha akaanza kama kulia ivi. Sikulijali hilo nikamwambia tujadili jinsi ya kuandaa mazishi ya wale maiti wawili. Akasema nadhani itakua jambo la busara kama tutaenda kuzika kijijini kwenu kwani hata binti wa kazi tulimtoa huko. Tulikubaliana taratibu za kusafirisha maiti zikafanyika na tukafanikiwa kuwazika mwanangu na Dada wa watu ambae hakua na hatia yoyote.
Tulimaliza matanga na kila kitu kukamilika kisha tukarudi mjini baada ya wiki mbili. Tulipofika Peris aliripoti kazini na akawa anaendelea na kazi kama kawaida. Na mimi pia nikaamua kuifuatilia ile kesi kimpango wangu kwani mpaka mda huo unaisha nilikua bado sijarudishwa kazini. Nilianza kufuatilia kwa umakini mkubwa ambapo kuna siku niliamua kwenda kwenye ile nyumba ya majambazi. Nilifika pale na kuruka ukuta kwani geti lilikua na shoti. Baada ya kuingia ndani nikatoa mzura wa kuficha sura.
Nikauvaa, kisha nikavaa groves nikatoa silaha na kuanza kunyata mle ndani. Nilizunguka vyumba vingi bila kuona mafanikio yoyote labda hata kumwona mtu. Baada ya kuhakikisha nyumba haina mtu hata mmoja nikaanza sasa kupekua vitu ili kama kuna ushahidi nitaupata unisaidie. Nilianza chumba fulani hicho sikuona vitu vya maana. Nikatoka na kuingia kingine humo nikaona kuna shoti za umeme, bunduki aina ya SMG, nyingi sana, Kulikua na vipisi vya nondo, zaidi kulikua na mabomu ya kutupa kwa mkono.Sare za jeshi la wanachi JWTZ, Pia na silaha mbalimbali za kisasa.
Hakika hili kundi walikua wamejipanga haswaa, hivi ndivyo nchi yetu inaendeshwa na watu wenye uwezo wa kuliendesha jeshi la polisi, Baada ya hapo nikatoka kuna chumba niliingia humu mlikua mnanuka uvundo. Nilifunuafunua nguo zilizokuwamo mle ndani nikakutana na maiti. Hali hii nilikutana nayo pia kule kwenye handaki kule ufukweni. Niliumia sana kuona maiti zikiwa zimepasuliwa na kutolewa utumbo wote. Hii ilikua ikiwapa nafasi wakati wakisafirisha madawa wanakua wamebeba mengi sana kwa mkupuo. Niliamua kutoka kwani uchungu ulikua unanizidi.Nikaamua kuingia chumba kingine huku nilikutana na vitu vingi sana. Kwanza kulikua na kabati lililokua limefungwa vizuri. Nilivunja kabati lile na kuanza kutoa kitu kimoja baada ya kingine.
Nilikutana na sura za bandia 12, na pia nilikutana na vinasa sauti vya kila namna vyenye thamani ya juu sana pia nilikutana na picha za watu waliopo kwenye orodha ya kuuawa, Alikuwepo mkuu wa kituo aliyeuawa tayari, pia alik uwepo Juma, Zaidi nikaona kiongozi mkubwa sana wa Jeshi la polisi akiwa kwenye orodha ile. Kichwa kilichanganyikiwa kwani pale wengine niliona wakiwa tayari wamekwisha uawa. Lakini kikinitisha ni idadi ya watu tena wengi walikua bado. Wengine nilikua nawafahamu na wengine siwafahamu.
Nilijiuliza kwanini wale watu wanataka kuangamiza idadi kubwa vile ya watu? Nilobaki nimeduwaa. Wakati naendelea kuangalia picha pia nikaiona picha yangu ikiwa imewekwa mwishoni kisha imeandikwa "most wanted" Nilishtuka sana lakini ningefanya nini unadhani. Nikazidi kukagua na kupekua mle ndani huku nikizidi kushuhudia vitu vingi na vya kuti. Mara kwa ghafla nikahisi mtu ananigusa bega moyo ukadunda kwa woga. Nikaanza kugeuka taratibu______________________
SEHEMU YA 21.
Tulipoishia Nikazidi kukagua na kupekua mle ndani huku nikizidi kushuhudia vitu vingi na vya kuti. Mara kwa ghafla nikahisi mtu ananigusa bega moyo ukadunda kwa woga. Nikaanza kugeuka taratibu____Endelea.....Kisha nikakutana na mtu akiwa amevalia mzura wa kuficha uso ili asigundulike. Alikua amejazia mwili kwani niliona kwa urahisi kutokana na nguo alizokua amevaa. Basi nikiwa najaribu kutafakari nifanye nini kwa mbele nikakiona kitu kama nondo imechongoka. Niliichukua haraka na kumdunga nayo tumboni bila huruma. Nilishuhudia utumbo ukitoka kwa macho yangu. Sikua na ujanja ikabidi nimfunue sura nimwangalie. Mungu wangu sikuamini ninachokiona.
Alikua ni miongoni ma maaskari ambao nimewahi kukutana naye katika kazi mbalimbali. Hakua kituo kimoja na mimi bali kingine. Lakini nilikua nakutana naye katika matukio mbalimbali ya kupinga ugaidi na ujambazi. Nilishtuka sana nikajiuliza je na huyu ni miongoni mwao au naye alihisi mimi ni jambazi? Yote kwa yote tayari nimeua hilo anajua Mungu. Nikaona mahali pale si salama tena nikaamua kuondoka na baadhi ya vitu. Nikatoka na kupotea eneo lile mara moja. Wakati nafika nyumbani nikakaa na kuzidi kutafakari juu ya yale ninayoyaona. Ikumbukwe pia kazi nlikua nimesimamishwa kwa mda. Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa Peris kukagua pia kwani nilishamtilia mashaka.
Sikutaka kupoteza mda nikampigia simu Peris ili nijue yuko wapi ili nifanye kazi yangu kwa uhakika. Alinijibu kua yuko kazini hapo ndipo nikaamua kuwasha pikpiki yangu na kupotea nyumbani kwangu kwa mwendo wa kasi sana. Nilifika kwa Peris na kupaki pikipiki nje kisha nikawa naingia. Lakini wakati naingia kuna mtu nikamwona mle ndani. Nikajisemea leo ndiyo leo yule ni nani na hapa tulihama. Naua mtu potelea mbali kesi ngapi zimenikuta? Nikatoa kisu chamgu kirefu kiasi kikali kilichokua kinakata kotekote, kilikua kinang'aa sana. Nikajiweka tayari. Kwa bahati mbaya naye akanishtukia. Aliponiona akaanza kuchukua tahadhari. Alikua na nywele ndefu nilikua namwona kupitia madirisha. Hali ile ilinifanya nijue ya kua ni mtu wa jinsia ya kike. Nikazidi kujisogeza ndani nikinyata. Mara akatoka kwa kasi ya ajabu.
Siachi mtu roho yangu ikajisemea. Nikaanza kumfukuzia. Alikimbia sana yule mwanamke na mpaja namfukuzia nilikua sijajua ni nani? Alikua na mbio kama mtu aliyekua amepitia mafunzo ya kijasusi. Askari mzima nilitolewa jasho. Sikutaka kumwacha kwani nilshapanga kutimiza azma yangu.Alikimbia mpaka barabarani. Sikutaka kukata tamaa nikazidi kumfuata mara akaingia vichochoro vya mtaa fulani pale Dar es salaam. Nikaamua kumfuata hadi huko. Alifika sehemu kuna ukuta akaruka hapo ndipo alinipoteza kwani biliporuka na mimi sikumwona mtu.
Niliangaza macho huku na kule sikuona kitu. Nikalaani sana. Nikaamua kurudi nyumbani kwa Peris. Baada ya kufika kwa Peris nilikua nimechoka sana lakini kile hakikua kikwazo cha kuifanya kazi yangu iliyonipeleka. Nikaingia ndani na kuanza mara mojaukaguzi. Kwanza hali niliyoikuta mle ndani ilikua ikionyesha kua mle ndani kuna shughuli hua zinaendelea kila uchwao. Japo tangu Peris kuhama pale hakuwahi kunambia kama anaenda pale. Hivyo hali ile ilikua ni kiashiria tosha ya kua pale mahali si salama.
Kwakua mtaka cha uvunguni sharti ainame ilinibidi nife kiume. Sikujali hatari yoyote mbele yangu. Nimaanza ukaguzi. Niliona kuna vitu kadhaa navitilia mashaka nikavikusanya. Mara kwa mbaali nikaiona "handbag" ya Peris. Nikaiendea na kuanza kuifungua. Wakati namaliza nilikutana na bastola mbili haikua ajabu kwa afande kua na bastola kilichonishitua ni kua zile bastola zilikua Hazijasajiliwa. Nikajiuliza kwanini? Nikaziweka chini na kuendelea na ukaguzi mara nikakutana na sura tatu za bandia. Pia mlikua na vichupa ful ani. Hivi vilikua na sumu kali sana.
Zaidi nikaona simu aina ya TECNO ikiwa iko hwani. Nikajaribu kuipiga kwangu ili nione jina litakalokuja. Baada ya kupiga kwangu nilishangaa simu yangu ikiwa inaita bila kuonyesha jina. Hali ile ilikua inanikumbusha miongoni mwa mbinu za Zabroni. Tayari nikaanza kupata muunganiko wa mambo. Tayari nikajua Peris huenda si mtu mzuri katika jeshi la polisi. Zaidi nikakutana na "Notebook" Bila ubishi mwandiko uliokuwamo ndani ulikua wa Peris.
Niliposoma vilivyoandikwa ndani Mungu wangu haikua rahisi kuamini. Niliona orodha ya nauaji yaliyotekelezwa na pia mengine bado. Nilishtuka zaidi pale nilipoona hata najina ya "house girl" wetu na mwanetu yakiwamo. Mbaya zaidi yalikua yakionyesha tarehe, mahali na mda wa kuua na jinsia ya muuaji. Nilibaki nimeachama mdomo kwa mshangao. Kumbe Peris ni chui aliyejivika ngozi ya mwanakondoo. Aaaah aaaaah hakika nimeingiliwa. Anajua mtoto anauawa na hafanyi chochote kwanini nilikuamini Peris kwanini?
Hali ile ilinifanya nishindwe kuendelea na ukaguzi kwani uchungu ulinizidia. Nikaamua kubeba vile vitu na kuondoka nyumbani kwa Peris. Nilipofika nyumbani mda ulikua umekwenda sana. Nilipaki pikipiki yangu na kuungua mlango. Chaajabu nilipoingia nikakuta bahasha mezani. Iliandikwa "KWAKO AFANDE YUU" Baada ya kuifungua nikakutana na "Cd" nikaichukua na kuiweka kwenye Laptop yangu. Mara kilichokua kinaonekana kilikua kinanishangaza sana.
Nilikua najiona mimi mwenyewe nikiwa nahangaika kiruka ukuta. Hapa ilikua ni kwenye ile nyumba ya majambazi. Shughuli zote nilizozifanya mule ndani ya jumba lile zilionekana huku mimi nikiwa naingia chumba hiki na kile. Moyo ulianza kwenda kasi huku nikijiona mjinga kwani nilirekodiwa bila ya mimi kujijua. Haaah hakika watu wale walikua wameendelea sana kiulinzi. Ulinzi wao ulizidi hata wa vituo vyetu vya polisi. Nilijiona matukio yangu yote hadi lile la kumuua mtu kwa kumchoma na nondo tumboni. Mpaka naondoka katika lile jumba. Mwisho wa ile video yakatokea maandishi "BROUGHT TO YOU BY ZABRONI MAKWEKA COMPANY" Nikameza mate funda moja.mara nikasikia mlango unagongwa ngo! Ngo! Ngk!__________________________
Maoni ushauri, Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment