» » Polisi wengine 5 wauawa katika shambulio Kenya


Maafisa wengine wane waliuawa katika eneo lililopo karibu na hilo siku ya JumnatatuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaafisa wengine wane waliuawa katika eneo lililopo karibu na hilo siku ya Jumnatatu
Maafisa watano wa polisi nchini Kenya wameuawa baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa barabarani kaskazini mashariki mwa mji wa Liboi karibu na mpaka na Somalia.
Shambulio hilo lilitokea karibu na eneo lile lile ambapo maafisa wengine wanne waliuawa katika shambulio jingine la bomu siku ya Jumatano ambalo kundi la Alshabab limekiri kutekeleza.
Maafisa wengine watano waliuawa katika mashambulio tofauti ya mabomu siku ya Jumatatu katika kaunti Jirani ya Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab limefanya mashambulio kadhaa nchini Kenya katika siku za hivi karibuni.
Kundi hilo lenye makao yake makuu Somali linataka Kenya kuondoa majeshi yake yanayohudumu chini ya vikosi vya AMISOM.
Mwandishi wa BBC Mohammud Ali mjini Nairobi ameripoti kwamba shambulio hilo la Mandera lililenga gari la gavana wa kaunti hiyo Ali Roba.
Bwana Roba alichapisha katika ujumbe wake wa Facebook siku ya Jumatatu kwamba alipoteza mlinzi wake katika shambulio hilo.
Ni shambulio la tatu ambalo lilimlenga Ali Roba katika kipindi cha siku tatu.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...