» » Obama alimuonya Trump kuhusu Flynn


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLuteni Jenerali mstaafu Mmmichael Flynn alikuwa ameteuliwa kuwa mshauri wa maswala ya kisiasa wa bwana Trump

Rais Barrack Obama alimuonya rais mpya wa Marekani Donald Trump dhidi ya kumteua Michael Flynn kuwa mshauri wake wa maswala ya usalama wa kitaifa , ikulu ya Whitehouse imethibitisha.

Bwana Obama alimuonya mrithi wake chini ya saa 48 baada ya uchaguzi wa mwezi Novemba wakati wa mazungumzo katika afisi ya rais, waliokuwa maafisa wa Obama wamesema.

Mawasiliano ya bwana Flynn na mjumbe mmoja wa Urusi yalimfanya kuwa rahisi kufanya usaliti jopo la seneti liliarifiwa siku ya Jumatatu.

Alifutwa kazi mnamo mwezi Februari kwa kuficha mawasiliano hayo.

Bwana Flynn ambaye ni luteni jenerali aliyestaafu aliudanganya utawala wa Trump kuhusu kuzungumza vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi na mjumbe wa taifa hilo Sergei Kislyak kabla ya Trump kuidhinishwa kuwa rais.

Katibu wa maswala ya habari Sean Spiecer alisema kwamba ni kweli rais Obama aliweka wazi kwamba hakumpendelea Jenerali Flynn.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...