» » Tanzania vyatangazwa Mexico Vivutio vyake


Haki miliki ya pichaISTOCKImage captionMmoja wa viongozi wa vijana wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa (kulia), akilakiwa na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam

Kiongozi wa vijana wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa amefanya kazi kubwa ya kuwashawishi Wananchi wa Mexico kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania badala Kenya.

Dk. Mutasingwa ambaye alikuwa nchini Mexico kwa mafunzo ya miezi minne ya kubadilishana uzoefu katika nyanja za utamaduni na uongozi alitumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, alisema kuwa moja ya mambo yaliyompa wakati mgumu ni kuwabadilisha wamexico kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya kama wanavyofahamu wao.

Alisema Wamexico wengi kwanza wanajua Afrika ni nchi, jambo ambalo pia ilibidi awaeleze kuwa siyo nchi bali ni bara kama yalivyo mabara mengine duniani na katika bara hilo kuna nchi nyingi na mojawapo ni Tanzania anayotokea yeye.

Alisema akiwa huko licha ya kuwafundisha kiswahili pia alitangaza vivutio vingi vya utalii vilivyopo nchini, ambapo aliwatajia wadudu, ndege wa kila aina na wanyama mbalimbali waliomo kwenye hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na nyinginezo.Pia aliwafundisha kuhusu utamaduni wa Tanzania zikiwemo ngoma za asili, upikaji wa vyakula vya kitanzania kama vile ndizi na pilau, mambo ambayo walifurahishwa nayo.

Dk. Mutasingwa alisema kuwa katika ziara hiyo ya mafunzo alikuwa na vijana wenzie wa Girl Guids kutoka Venezuela, Canada, Uingereza na Argentina na kwamba alipata wasaa wa kujifunza utamaduni wa mexico na kutoka nchi hizo zingine.Alisema kuwa alijifunza mambo mengi ikiwemo ujasiri wa kufanya kazi bila woga, siasa za mataifa mbalimbali, mambo ambayo ameahidi kuwafundisha vijana wenzie wa TGGA nchini Tanzania.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...