» » MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA WILAYANI UBUNGO UKITOKEA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kisare Makori amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi tayari kwa kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo katika Manispaa ya Ubungo.

Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umezuru kwa Mara ya Kwanza katika Wilaya mpya ya Ubungo hivyo historia mpya imeandikwa.

Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Kwa Mwaka 2017 katika Wilaya ya Ubungo utakimbizwa umbali wa Kilomita 46 na  gharama ya Miradi yote Mwenge utakapopita ni Zaidi ya Bilioni 2.8

Mwenge wa Uhuru Mwenye kauli mbiu ya kutilia msisitizo kushiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo ile ya Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, tuwajali na tuwasikilize watoto na vijana utakapomaliza kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Ubungo utaelekea Mkoani Pwani.

Katika mbio za Mwenge Umebaba ujumbe mwingine wa kuhamasisha kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

Aidha watanzania wameombwa kushiriki kutokomeza Malaria kwa Manufaa ya Watanzia na jamii kwa ujumla.

Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...