Shinikizo hazitamlazimisha meneja wa muda mrefu wa Arsenal Arsene Wenger ajiuzulu, beki wa zamani wa klabu hiyo Laurena mesema.
Arsenal watakutana na Southampton katika Ligi ya Premia Jumatano jioni na iwapo watashinda huenda wakapanda hadi nafasi ya tano.
Mkataba wa Mfaransa huyo unafikia kikomo mwisho wa msimu huu na amekosolewa sana msimu huu kutokana na matokeo ya klabu hiyo.
- Wenger: Nina kinga dhidi ya ukosoaji mbaya
- Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi
- Mourinho: Wenger na Klopp hawana ''maadili''
- Mourinho: Nafurahi mashabiki wa Arsenal walifurahi
Lauren, 40, aliambia BBC Africa: "Anafahamu kukabiliana na presha, natumai kwamba mambo yatakuwa sawa hivi karibuni."
Lauren alichezea Arsenal mechi 159 ligini kati ya 2000 na 2007 na alikuwa kwenye kikosi kinachosifiwa sana cha "invincibles" (Wasioshindwa) ambacho kilishinda taji la ligi mwaka 2003-2004.
Beki huyo wa kulia wa zamani wa Cameroon alisema: "Sidhani (Wenger) atajiuzulu. Amekabiliwa na shinikizo kwa miaka 30-35, akisimamia klabu kubwa zinazokabiliwa na presha."
Februari, Wenger alisema angeamua kuhusu mkataba mpya Machi au Aprili lakini baadaye alisema labda alifanya kosa kwa kuahidi watu kwamba angekuwa ameamua hatima yake katika kipindi hicho.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment