» » Diamond TRA Yafafanua kuhusu kudaiwa Kodi ya Milioni 400

Mkurugenzi wa  Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.

Hayo ameyasema jana Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi anayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahati nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. 

Awali akifungua semina hiyo, Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi,Alisema Bw. Kayombo.

Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...