» » Lowassa Alaani Kongamano la demokrasia Kuzuiwa

Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amelaani vikali kitendo cha serikali ya Mkoa wa Dar es salam kuzuia kongamano la demokrasia lililopangwa kufanyika siku ya jana may 13, Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Mhe. Lowassa jana  akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni, Dar alisema kuwa amesikitishwa sana na serikali kuzuia kongamano ambalo lilikuwa na nia njema ya kuzungumza kuhusu demokrasia na kujifunza kutoka kwa watu mbali mbali jinsi ya kufanya siasa bila kukosea na kurekebishana penye makosa.

Mjumbe huyo aliendelea kufafanua kwamba hakuna tatizo kwa vyama vya siasa kutofautiana mawazo kwani ndiyo demokrasia na ndiyo sababu kubwa  ya waandaji kushirikisha watu wenye taaluma tofauti tofauti katika kongamano hilo.

"Chadema kwa ujumla tunalaani sana kitendo cha Serikali ya Dar es salaam kuzuia mkutano wa amani wa kuwaunganisha watanzania pamoja kwa kutumia kongamano la demokrasia. 

"Kitendo ambacho kimefanywa  ni kuminya demokrasia. Nia ilikuwa njema na ndio maana waandaji wa kongamano waliweka picha yangu na kinana tukiwa tunatabasamu hivyo hakuna dhambi kwenye kutofautiana mawazo"- alisema Lowassa.
Taarifa iliyotolewa jana kuhusu kongamano.

Hata hivyo Mhe. Lowassa amekitaka chama cha Mapinduzi kutonyayasa upinzani kwa kuwa hawataweza kukaa madarakani muda wote huku akiwatahadharisha wakumbuke vyama vya ukombozi wa Afrika vilivyobaki madarakani ni  ANC na CCM.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...