» » Madai ya mipango ya Rais Zuma kuhamia Dubai yaibuka Afrika Kusini

Je, Rais Zuma ana mipango ya kuhamia Dubai?

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJe, Rais Zuma ana mipango ya kuhamia Dubai?
Nchini Afrika kusini kashfa mpya inatokota inayozingira madai ya rais Jacob Zuma ya kuzingatia kuhamia Dubai.
Barua pepe hizo zimechapishwa na gazeti moja nchini Afrika kusini na zinaonyesha uhusiano mkubwa kati ya rais wa Afrika kuisni Jacob Zuma na familia yenye utata, Gupta, hususan kuhusu madai kwamba rais Zuma anazingatia kuhamia Dubai.
Wakati chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani, barua pepe hizo zinatarajiwa kuibua mjadala mkali kwani zinafichua mipango ya rais Zuma ya kuhamia Dubai.
Barua pepe hizo baina ya mwanawe Zuma, Duduzane, na vigogo wa kampuni inayomilikiwa na familia tatanishi ya Gupta, zinashirikisha barua moja iliyotumwa kwa familia ya kifalme nchini Dubai, ambapo Zuma anasema angetaka kuwa na makao ya pili huko Dubai.
Madai hayo yanaibua mjadala wa iwapo rais Zuma anajiandaa kubwaga manyanga kwani chama cha ANC kinaonekana kumgeuka.
Zuma amekumbwa na kashfa nyingi ikiwemo ya makao ya NkandlaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionZuma amekumbwa na kashfa nyingi ikiwemo ya makao ya Nkandla
Msemaji wa rais amepuuza barua pepe hizo kama uvumi na uchokozi.
Hayo yakiarifiwa, ombi la kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma limewasilishwa kwa kamati kuu ya chama cha ANC inayokongamana mjini Pretoria.
Ni mara ya pili sasa ambapo waasi wa chama hicho wanawasilisha ombi hilo.
Hata hivyo, huenda wanchama wa kamati hiyo watiifu kwa rais Zuma wakaangusha mswada huo.
Kwa sasa kesi inaendelea katika mahakama ya kikatiba ya iwapo wabunge wa Afrika kusini watapiga kura ya siri ya kwa mswada wa kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma.
Kamati hiyo inatarajiwa kuamua atakayemridhi bwana zuma mwezi Desemba.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...