» » Askofu Gwajima Afunguka Mazito Sakata la Madini Katika Mchanga

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma.

Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali nyingi

"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima

Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo

"Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda" alisema Gwajima


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...