Trump aionya tena Korea Kaskazini
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionMeli ya Carl Vinson kwa sasa inaelekea rasi ya Korea
Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa onyo dhidi ya Korea Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Pyongyang inatafuta matatizo.
Pia aliitaka China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.
Bwana Trump alipendekeza kuwa China itapata makubaliano bora ya kibiashara ikiwa itafanya hivyo, lakini akaongeza kuwa Marekani haitaogopa kutatua tatizo la Korea Kaskazini bila ya Uchina.
Marekani yapeleka meli za kivita katika rasi ya KoreaWakazi Japan wajiandaa dhidi ya Korea KaskaziniJe dunia itaifanya nini Korea Kaskazini?Korea Kaskazini yafyatua kombora upande wa Japan
Bwana Trump alitoa matamshi kama hayo wiki moja iliyopita lakini tangu wakati huo msukosuko umekuwa mkubwa.
Marekani imetuma meli za kivita kuenda kwa maji ya rasi ya Korea hatua ambayo imeighadhabisha Korea Kaskazini.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMeli ya Carl Vinson hubeba ndege aina ya F/A-18F Super Hornets
Mshirikishe mwenzako

No comments:
Post a Comment