» » Mataifa ya G7 yakataa kuiwekea Urusi vikwazo baada ya shambulizi la kemikali Syria

Mataifa ya G7 yakataa kuiwekea Urusi vikwazo baada ya shambulizi la kemikali Syria

Haki miliki ya pichaEPAImage captionShambulizi la Khan Sheikhoun liliwaua watu 89

Mataifa tajiri duniani ya G7 yamekataa ombi la Uingereza la kutaka vikwazo kuwekwa dhidi ya Urusi baada ya shambulizi baya la kemikali linaloaminiwa kuendeshwa na mshirika wa Urusi, Syria.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi alisema kuwa kundi la G7 halikuwa na nia ya kuisukuma Urusi kuenda kwa ukuta na badaa yake lilitaka kuwepo mazungumzo.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, kwa sasa anafunga safari kutoka nchini Italia kwa mazungzo mjini Moscow.

Urusi: silaha za kemikali zilizowaua watu Syria ni za waasiUrusi yatakiwa kuacha kumuunga mkono Bashar al-Assad

Amesema kuwa rasi wa Syria hawezi kushirii katika mchakato kuhusu hatma ya nchi.

Siku ya Jumanne bwana Putin aliutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchuzi huru kuhusu shambulizi la kemikali, katika mji unaodhibitiwa na waasikwenye mji wa Khan Sheikhoun lililowaua watu 89.

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRex Tillerson (kulia) anaelekea mjini Moscow

Alisema pia kuwa amesikia kuwa mashambulizi bandia yanafanywa ili kuiwekea lawana serikali ya Syria.

Syria ilikana kufanya shambulizi hilo, lakini Marekani ilijibu kwa kufyatua makombora kuenda kwa kambi ya wanahewa nchini Syria.

Urusi yashutumu shambulio la Marekani dhidi ya Syria

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Italia Angelino Alfano, ambaye aliandaa mkutano wa G7 katika mji wa Lucca, alisema kuwa mawaziri hao walitaka kuzungumza a na Urusi kuitaka imushinikize rais wa Syria Bashar al-Assad baadla ya kuisukuma Urusi hadi kwa ukuta.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionJeshi la Syria linasema kuwa uharibifu katika kambi ya wanahewa haukuwa mkubwa

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles