» » Thabo Mbeki aunga mkono wapinzani wa Zuma

Thabo Mbeki aunga mkono wapinzani wa Zuma

Haki miliki ya pichaAFPImage captionThabo Mbeki alijiuzulu kama rais wa Afrika Kusini mwaka wa 2008.

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki anawataka wabunge wa chama cha ANC kutenda yatakayowafaa raia na sio kile kitakachofaidi chama, wakati wa kujadili mswada wa kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma, wiki ijayo.

Wito wa Mbeki huenda ukawakera wanaomuunga mkono Zuma ambao wameapa kuupinga mswada huo vikali bungeni, kulingana na tovuti ya IOL.

Upinzani unadai kuwa Zuma ni mfisadi na kuwa alimfuta kazi Pravin Gordhan kama waziri wa fedha, licha ya kuwa Gordhan aliheshimika sana.

Wanasema nia ya Zuma ilikuwa kuchukua usukani katika wizara ya fedha.

Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jelaRais Zuma aponea shinikizo za kumtaka ajiuzuluChama cha wafanyikazi chamtaka Zuma kujiuzulu

Zuma anakanusha madai ya ufisadi akisema kuwa yeye kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na ni kwa manufaa ya raia

Kulingana na tovuti hiyo, Mbeki alisema kuwa wabunge wanafaa kuwa sauti ya wananchi na wala sio sauti ya vyama vya kisiasa.

Anasema huu ni wakati wa Afrika Kusini kujua ukweli kuhusu uhusiano wa kikatiba kati ya wananchi na viongozi wao wa kisiasa.

Zuma amfukuza kazi waziri wa fedha Pravin GordhanMaandamano ya kumtimua rais Zuma mamlakani yaanza

Mbeki ni mwanachama wa ANC ambaye alijiuzulu kama rais baada ya kupoteza imani kwa chama hicho kinachoongozwa na Zuma, mwaka wa 2008.

Mada zinazohusiana

Jacob ZumaSiasaANCAfrika Kusini

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles