» » Rais Kabila,Wapinzani wazungungumzia mustakabali wa DRC

Rais Kabila,Wapinzani wazungungumzia mustakabali wa DRC

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRais Kabila

Rais Joseph Kabila ameanza mazungumzo na Mashirika ya kiraia na wanasiasa wa upinzani kuhusu mustakabali wa siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kushindwa kufikia maamuzi, mazungunzo yaliyokuwa yakiongozwa na maaskofu wa kanisa katoliki.

Mpaka sasa chama tawala na upinzani wameshindwa kuafikiana kuhusu uteuzi wa waziri mkuu ,Mazungumzo haya mapya wanatarajia jibu la rais Joseph Kabila kwa maskofu wa kanisa katoliki ambao walijaribu kupatanisha wanasiasa wa upinzani na wa chama tawala kwa muda wa miezi mitatu lakini jitihada zao zilishindikana.

Hata hivyo kufuatana na msimamo wa kila upande , wakishindwa kuafikiana kuhusu kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya ambae alipaswa kutoka upande wa upinzani baada ya kushindwa maskofu waliomba rais Joseph Kabila kujaribu mwenyewe kutautua mgororo huu lakini hadi sasa vyama vikuu vya upinzani vimemsusia rais huyo na kukataa kufanya uchaguzi .

Mjadala huu mpya unaweza kuchukua muda wa siku tatu na hapo baadae rais Kabila atatoa hotuba ya mwisho bungeni juu ya mgororo huo wa kisisisa.

Kwa sasa maeneo mengi ya nchi hiyo yako kwenye hali ya wasiwasi, huku baadhi ya shughuli mbalimbali mjini Kinshasa kusimama kama vile kufungwa kwa baadhi ya maduka,shule na baadhi ya ofisi .

Wasiwasi DR Congo muhula wa Kabila ukifikia kikomoUpinzani na serikali waafikiana DRC

Mshirikishe mwenzako 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles