Mshauri mkuu wa kiongozi wa Taleban auawa na Marekani

Makao makuu ya jeshi ya Marekani, Pentagon, yamemlenga na kumwua mshauri mkuu wa kiongozi wa Taliban, Abu Bakr al -Bhagdadi katika shambulio lililofanywa nchini Syria.
Msemaji wa Pentagon, kanali John Thomas, alisema kuwa Abdul Rahman al-Uzbek, aliuawa Aprili 6 lakini hakutoa taarifa zaidi.
Alisema kuwa Al-Uzbeki alishiriki katika kupanga mashambulizi kwenye kilabu kimoja usiku wa kuamkia mwaka mpya mjini Istanbul ambako watu 30 walifariki.
- Watu 100 waliotekwa na Taleban waokolewa
- Wapiganaji waliovalia kama madaktari washambulia hospitali Kabul
- Kiongozi wa Taliban awataka watu kupanda miti Afghanistan
- Wanajeshi 100 wa Afghanistan wauawa katika shambulio
Mwandishi wa BBC alisema kuwa ingawa kuna wanajeshi zaidi ya 500 wa Marekani kutoka kikosi maalumu nchini Syria kwa kawaida hawashiriki katika oparesheni moja kwa moja.
Alisema wao hutumia muda mwingi kutoa ushauri kwa makundi asilia ya maeneo hayo jinsi ya kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:
Post a Comment