» » Mkutano wa CUF ya Maalim Seif Wavamiwa na Watu wenye Silaha......Wananchi Wafanikiwa Kumnasa mmoja

Mkutano wa CUF ya Maalim Seif Wavamiwa na Watu wenye Silaha......Wananchi Wafanikiwa Kumnasa mmoja

Watu wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo.

Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.

Mtu huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na wenzake katika eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi huo katika mkutano wa wanachama wa CUF.

Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles