Kutokana na uhitaji wa Elimu ya maisha kwa vijana 4sn news utakuwa inakupatia masomo ya ndoa mahusiano kutoka Kwenye nukuu na vitabu mbali mbali hivyo wambie vijana wako marafiki zako ndugu na jamaa was Downlod bApps ya 4sn news IPO play store/Android ili wapate masomo hayo bure kabisa Kwenye Simu zao
SoMo la leo
CHAGUWA MAISHA SEHEM YA KWANZA
Andrew, David na Peter walilitazama kwa makini lori lililokuwa likipita kijijini mwao. “Unajua,” Andrew aliwaambia rafiki zake, "naomba niwe na gari siku moja. Nitapenda kuendesha gari kila mahali. Sijui itanilazimu kuwa na misimu mingapi ya mavuno ili niweze kupata fedha za kununua gari dogo la mizigo nianze kufanya biashara" "Mimi sipendi kupata gari dogo la mizigo," David alijibu. "Ndoto yangu ni kuendelea na masomo hadi Chuo Kikuu ili niwe Daktari. Nimeshuhudia vile wazazi wangu walivyohangaika kupata chakula na karo ya shule. Nawaheshimu kwa kazi yao kubwa, nawashukuru kwa vile walivyojitolea mhanga ili sisi watoto wao tusome. Lakini sipendi kufanyakazi shambani kutwa nzima kama wao. Ningependa niwe na zahanati ili niweze kuwasaidia wananchi na wakati huo huo niweze kuisadia familia yangu." "Hilo ni wazo zuri sana David," Peter alisema. "Lakini mimi sipendi kusoma tu kila wakati. Tutakapofuzu masomo yetu ya shule ya upili mwaka ujao, sitaendelea na masomo tena. Sipendi kuachana na maisha ya mashambani. Ninaipenda sana milima hii, hapa ndipo ningependa kuishi. Ndoto yangu ni kuwa na nyumba nzuri, mke anayenipenda, watoto sita pamoja na kundi la ng'ombe. Iwapo nitakuwa na hivi vyote, nitakuwa na furaha ya ajabu." "Lakini," Peter aliendelea kusema, "Alex yuko wapi? Sijamwona kwa majuma kadhaa sasa." "Hujui?" Andrew alijibu. "Alilazimika kukatisha masomo yake, kwa sababu familia yake haikuwa na uwezo wa kumlipia karo ya shule. Baba yake ameugua kwa muda mrefu na hali yake imekuwa mbaya zaidi. Hivi sasa familia inatumia fedha yote kwa ajili ya matibabu yake. Alex hajui maisha yake ya baadaye yatakuwa vipi. Alikuwa akiongoza katika somo la hesabu darasani mwetu na amekuwa akitarajia kuwa mara tu amalizapo shule ya upili, atachukua kosi ya komputa. Angependa pia kuwa mhasibu. Lakini iwapo baba yake atafariki, ana mashaka kama ataendelea na masomo yake, na atakabiliwa na jukumu kubwa la kuwatunza mama yake, ndugu na dada zake."
MAMBO YAKUJADILIANA 1)
Vijana hawa walikuwa na ndoto gani? 2) Kila kijana alitakiwa kufanya uchaguo gani ili kutimiza ndoto yake? 3) Ni uchaguo gani ungewasaidia kuepuka na mambo yasiyoweza kuwafanya watimize ndoto zao? 4) Unafikiri kuwa Alex anaweza kutimiza ndoto zake endapo baba yake atafariki? Ikiwa ndiyo, anaweza kutimiza kwa njia gani?
KESHO LITAENDELEA.

No comments:
Post a Comment