» » Maporomoko ya ardhi yaua watoto 44 Colombia

Maporomoko ya ardhi yaua watoto 44 Colombia

Vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta walionusurikaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionVikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta walionusurika
Raia wa Colombia walionusurika kwenye ajali ya maporomoko ya ardhi katika mji ulio kusini mwa nchi hiyo Mocoa, wamekuwa wakifukua vifusi kuwatafuta watu ambao mpaka sasa hawajulikani walipo.
Asilimia 30 ya mji huo umeathiriwa na maporomoko hayo.
Watu 254 wanaelezwa kupoteza maisha kwenye tukio hilo baya siku ya ijumaa Dimitri O' Donnell ni mwandishi wa Habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bogota
'' Katika kipindi cha saa tatu , asilimia 30 ya mvua ambayo hunyesha mjini Mocoa, kwa mwezi ilinyesha kwa saa hizo tatu, kiasi ambacho kingenyesha kwa siku takriban 10, kwa hiyo ilikua mvua ya kumshtua kila mtu''
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ambaye anautembelea mji wa Mocoa kwa siku mbili sasa amesema zaidi zaidi ya watu 200 wamebainika kupoteza maisha, miongoni mwao watoto 44. idadi zaidi ya waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka kwa kuwa bado watu takriban 300 bado hawajulikani walipo.
Mwanabaiolojia Carolina Pardo kutoka chuo kikuu cha El Rosario mjini Bogota,amezungumza na BBC akisema matumizi mabaya ya ardhi yamesababisha mmomonyoko wa udongo uliosababisha maporomoko ya ardhi.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles