» » Algeria kuweka picha za wagombea wa kike

Algeria kuweka picha za wagombea wa kike

Haki miliki ya pichaHIZB AL ADAL WAL BAYANImage captionMabango ya kampeini Algeria

Vyama vya kisiasa nchini Algeria vimeridhia kuweka picha za wagombea wa kike kwenye mabango yake.

Vyama vingi vimekua vikiweka picha za mitandio bila kuwepo na uso wa mgombea.

Hata hivyo picha za wagombea wa kiume zimetawala kwenye mabango.

Maafisa wa uchaguzi wameagiza vyama kuanza kuweka picha za wagombea wa kike la sivyo vitaondolewa kwenye usajili.

Hatua hii imevutia hisia tofauti kutoka kwa wagombea wa kika na kiume.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMabango ya kampeini Algeria

Mmoja wa wagombea Fatma Tirbakh wa chama cha 'National Front For Justice' amesema eneo anakotoka kuna mila na itikadi kali dhidi ya wanawake kujionyesha hadharani.

Hata hivyo amesema anataka picha yake kuwekwa kwa bango, kinyume na awali ambapo ni jina tu lililowekwa.

Chini ya sheria ya mwaka 2012, nchini Algeria, vyama vya kisiasa vinatakiwa kuwateuwa kati ya asili mia 20 na 50 ya wanawake kama wagombea.

Algeria siyo taifa pekee ambapo wagombea wa kike hawaweki picha zao kwenye mabango wakati wa kampeini.

Nchini Misri vyama vyenye itikadi kali za kidini vilitumia picha ya maua badala ya picha za wagombea wa kike kwenye uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2011 na 2012.

Mada zinazohusiana

AlgeriaWanawake

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...