» » Mkenya Sarah Ikumu ashangaza kwa kipaji Britain's Got Talent Uingereza

Mkenya Sarah Ikumu ashangaza kwa kipaji Britain's Got Talent Uingereza

Haki miliki ya pichaSARAH IKUMU/ INSTAGRAM

Kijana Mwingereza ambaye wazazi wake Wakenya amevuma sana mtandaoni baada ya kusisimua kwa wimbo katika shindano la vipaji katika sanaa Uingereza la Britain's Got Talent Jumamosi.

Sarah Ikumu, 16, aliyezaliwa Uingereza, aliwashangaza wengi katika kipindi cha vipaji cha Britain's Got Talent, alipoimba wimbo wa And I'm Telling You ambao unadaiwa kuwa mgumu sana kuuimbwa ipasavyo.

Wimbo huo wake Jennifer Holliday ulitumiwa kwenye filamu ya Dreamgirls iliyotolewa mwaka 2006.

Uimbaji wa Sarah uliwaacha waliohudhuria mashindano hayo wakiwa wameduwaa huku wote wakisimama na kumshangilia.

Kilele cha uimbaji wake kikifika pale mmoja wa majaji ambaye anajulikana kuwa mgumu kufurahisha, Simon Cowell, alipobonyeza kengele ya dhahabu ambayo humpeleka mshiriki moja kwa moja hadi nusu fainali ya mashindano hayo.

Daktari Mtanzania atambuliwa Marekani

Sarah ambaye anasomea Milton Keynes alianza kuimba akiwa na miaka mitano huku akishiriki kwa mashindano kadha ya nyimbo.

Lakini hili ndilo shindano la kwanza ambalo anasema kuwa ni ndoto ambayo imetimia, mwanzo pale Jaji Simon alipompongeza kwa talanta yake akimuambia "lilikuwa jambo la kushangaza kwa mtu rika lake kusimama mbele ya watu akiwa na hofu na kuelekea kuimba wimbo ni kama ameutunga mwenyewe".

Mwimbaji mashuhuri ambaye pia ni jaji Alesha Dixon alimwambia Sara kuwa "'hakubaliwi' kuwa na talanta kama hii katika umri wake"

Majaji wengine wawili wakiwemo David Williams, Amanda Holden pia walimmiminia pongezi.

Mitandao ya kijamii ilifurika watu wakimsifu.

Mada zinazohusiana

UingerezaSanaaKenyaWanawake

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...