Zuma amfukuza kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan
Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpyaSambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako
Image captionKwa siku za hivi karibuni Zuma amekuwa na ushawishi mdogo ndani na nje ya chama cha ANC
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya.
Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.
Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.
Image captionAliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordhan
Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.
Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan.
Mshirikishe mwenzako

No comments:
Post a Comment