» » Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba Aagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye Achukuliwe Hatua Kali za Kisheria

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba Aagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye Achukuliwe Hatua Kali za Kisheria

Kufuatia tukio la mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni Askari kumtishia Mbunge Nape Nnauye kwa kutumia bastola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema tukio lile halikuwa sahihi na kuagiza hatua zichukuliwe.

Waziri Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia usalama wa raia na mali zao amesema kuwa, Nape Nnauye si jambazi, hakuwahi kuwa na taarifa za uhalifu, sasa kwanini mtu amtishe kwa bastola tena mbele ya umati mkubwa uliojaa waandishi wa habari?

“Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.”

Aidha, Waziri Nchemba amesema kuwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kumbaini mtu huyo aliyefanya kitendo hicho na kumchukulia hatua stahiki.

“Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.”

Nape Nnauye alitishwa na bastola hiyo jana alipofika katika Hoteli ya Protea Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kumvua Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

==>Tazama video hii kuona ilivyokuwa

 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...