MHE ESTHER N. MATIKO AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI MTAA WA GIMENYA NA S/M BUGOSI
Mtaa wa Gimenya ni moja ya Mitaa inayounda kata ya Turwa iliyoko ndani ya Jimbo la Tarime Mjini. Ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha anawaletea maendeleo Wananchi wa Mtaa huo wa Gimenya na Jimbo la Tarime Mjini, Mhe Esther N. Matiko atimiza ahadi yake baada ya kuwakabidhi *Mifuko 40 ya Saruji.*
Itakumbukwa Mhe Matiko katika Ziara yake ya kutembelea Mitaa ya Jimbo la Tarime Mjini aliweza kufika ndani ya Mtaa huo na kuombwa kusaidia uanzishwaji wa ujenzi wa Ofisi ya Mtaa. Wanamtaa wa Buguti walimueleza Mhe Matiko wanampango wa kuanza kujenga Ofisi ya Mtaa itakayokuwa ni sehemu ya wao kupata huduma za Mtaa na sio kwenda kupata huduma hizo nyumbani kwa Mwenyekiti wa Mtaa.
_Baada ya kusikia kilio chao Mhe Matiko aliwahidi kuwapatia Mifuko 40 ya Saruji ili ujenzi wa Ofisi hiyo uanze haraka. Bila ajizi ndani ya wiki moja Mhe Matiko amerudi Mtaani hapo akiwa na Mifuko hiyo 40 ya Saruji na kuwakabidhi wanamtaa hao kwa ajili ya ujenzi._
Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Mtaa wa Gimenya, Mwenyekiti wa Mtaa huo (Sasita), amemshukuru sana Mhe Matiko na kusema haijawahi kutokea ndani ya Mtaa huo kwa viongozi waliopita kwa kutimiza ahadi zao ndani ya mda mfupi, Mwenyekiti wa Mtaa alisisitiza kuwa Mhe Matiko kaingia kwenye Historia ya Mtaa huo.
Mwenyekiti wa Mtaa alimwambia Mhe Matiko kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi hiyo ya Mtaa itakuwa ni faida kubwa sana kwani wataweza kumpata Mtendaji wa Mtaa atakayewasaidia kuhudumia wananchi na kuondokana na usumbufu wa kwenda kupata huduma za Mtendaji Katani.
Wote kwa pamoja wananchi wa Mtaa wa Gimenya walimshukuru sana Mhe Matiko na kuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anawaletea Maendeleo Wanatarime Mjini kwa kushirikiana na wadau wengine.
*_Ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha Tarime inasonga mbele katika Miundombinu ya Elimu, Mhe Matiko alifika shule ya Msingi Bugosi na kutimiza ahadi yake ya kuwapatia Mifuko 20 ya Saruji._*
Itakumbukwa shule ya Msingi Bugosi ni moja ya shule ambazo Mhe Matiko amepata kusahidiana na wananchi wa Mtaa wa Bugosi kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unasonga mbele kwa _kuwachangia Bati zilizohezeka choo cha Wanafunzi pia Mhe Matiko alipata kuwachangia Tofali 2000 zilizotumika kumalizia ujenzi wa darasa moja._
Lakini bado Mhe Matiko hajaishia katika hiyo michango yake, Safari hii baada ya kutoka Mtaa wa Gimenya Mhe Matiko amefika shuleni hapo na kuwakabidhi Mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Choo cha Walimu.
Shule ya Msingi Bugosi ni shule mpya inayojengwa kwa nguvu za wananchi, ili kupunguza makali ya kuchangishana Mhe Matiko kaamua kutoa mifuko hiyo ya Saruji aliyomkabidhi diwani wa Kata hiyo (Bashiri Abdalah), Mwalimu Mkuu, Mwenyekiti wa Mtaa na wananchi waliofika shuleni hapo ili ujenzi wa Choo hicho cha Walimu ukamlike haraka.
_Mhe Diwani alipata kuzungumza kwa niaba ya wananchi wake na kumshukuru Mhe Matiko kwa msaada huo na kumuomba hasichoke kupokea maombi yao pale watakapokuwa na uhitaji wowote wenye lengo la maendeleo._
Naye Mhe Matiko alipata kuwashukuru wananchi wa Bugosi kwa jitihada wanazozionyesha kwenye ujenzi wa shule hiyo na kuwahidi kuendelea kuwa nao bega kwa bega ili wanafunzi wa shule hiyo wapate mahala pazuri pa kujifunzia na walimu wa shule hiyo waweze kuwa na mahala pazuri pa kufundishia.
_"Tarime Yetu Mshikamano Kwa Wote"_
_"Rasirimali Zetu Kwa Maendeleo Yetu"_
*Imetolewa na :~*
*Peter Magwi Michael*
*Katibu wa Mbunge*
*Jimbo la Tarime Mjini*


No comments:
Post a Comment