» » Magufuli awatahadharisha wanahabari Tanzania

Magufuli awatahadharisha wanahabari Tanzania

Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIAImage captionDkt John Magufuli amewaambia wamiliki wa vyombo vya habari wasifikiri "wana uhuru" wa kufanya watakavyo

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa onyo kwa vyombo vya habari nchini humo kwa madai vinaandika habari zisizo za kizalendo.

Kiongozi huyo amemtaka waziri mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria.

"Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dkt Magufuli pia alimuapisha Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, na Bw Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.

"Kwa kuwa wewe ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache."

"Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, haya ndiyo mambo muhimu ya kuandika lakini hebu angalia siku iliyofuata jinsi magazeti yalivyoandika," amesema Dkt Magufuli.

Waziri ashutumu askari kwa kuchomoa bastola TanzaniaWaziri aliyetimuliwa Tanzania amwagiwa sifaMagufuli amfuta kazi waziri wa habari

Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba ukurasa wa juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akitolewa bastola katika vurugu zilizotokea jana.

Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIAImage captionDkt Magufuli akiongea na wanahabari ikulu baada ya kuwaapisha mawaziri wawili

"Hata kasomeni tu leo magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."

Mada zinazohusiana

Haki za KibinadamuTanzania

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...