USHINDI HATIMAYE- UTAZITAMBUAJE DINI ZA UONGO?
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
“Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo na watafanya ishara za ajabu na miujiza mingi ili kuwadanganya, hata ikiwezekana, wateule wa Mungu.”(Mathayo 24:24)
Tukiwa na maarifa ya kweli hatupaswa kushikwa na vitu visivyo hakika,mashaka,hofu au kukata tamaa maana dini haipimwi kwa wingi wa watu au umahiri wa watu kuongea bali Ukweli uliomo katika Biblia kwa kusoma na kutafakari. Dini ya uongo haina faida kwani uongoza kwenye uharibifu. Kwa hiyo, Wakristo wa kweli wapaswa kuepuka kila kitu kinachopatana na dini za uongo.Lazima ujue ukweli ndipo utajua uongo, vilevile, tukitambua dini ya kweli, tunaweza pia kutambua dini za uongo.
UKWELI KUHUSU DINI ZA UONGO
Wanakuwa na Kiongozi Mmoja kama masihi au mbadala wa Mungu.Kiongozi wao huchukuliwa kama ni mtu ambaye hakosei,ukristo wao ni wa maonesho,waumini humwogopa kiongozi wao. Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu, yeye ni msaada wetu daima.Yesu hakuogopwa bali alikuwa nani kimbilio la watu wote.
Huleta Mafundisho ya Kibinadamu badala ya Neno la Mungu.Biblia inasema “Watakase kwa neno lako; kwa maana neno lako ndilo kweli”(Yohana 17:17).
Dini ya uongo waumini hupumbazwa vichwa kwa kuvuruga ubongo kwa uwezo wao au umizimu. Kwa kuwa moyo usiokamilika wa mwanadamu unaweza kupotoshwa, tunahitaji kuchukua kwa uzito ushauri huu: “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo.” Na si ajabu, kwa maana Shetani mwenyewe huendelea kujigeuza mwenyewe kuwa malaika wa nuru.(2Korintho 11:14).
Hukazania Miujiza kuliko NENO la Mungu. Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, ataiamini Biblia na kuifanya kuwa msingi wa utendaji wake wote. Huduma yoyote ya miujiza isiyoambatana Biblia, inatokana na Shetani. Ni lazima iambatane na KUHUBIRI NA KUFUNDISHA Neno la Mungu kwa lengo la kuwaleta watu kwa Yesu,kukiri na kumpatia Mungu Utukufu.
Tabia nyingine ya dini za uongo,wanatenganisha watu na familia zao.Dini inayokuweka mbali na familia haina nuru.Wapo waumini wengine hawasalimiani na watu ambao wanadhani ni wadhambi lakini Yesu alichangamana na watu. Hakika ikiwa yeyote hawaandalii mahitaji wale walio wake mwenyewe, na hasa wale walio washiriki wa nyumba yake, ameikana Imani naye ni mbaya kuliko mtu asiye na imani. Njoo kwa Yesu,wokovu ni bure,Bwana akuita.Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi na kukupatia USHINDI HATIMAYE
Pakua App ya 4sn news kwa Android
Tuma habari picha 0659750504
No comments:
Post a Comment