USHINDI HATIMAYE- UTAMBUZI WA MTU SAHIHI
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
Mafungu:1 Samwel 30:9-12,13,15,17;Methal 16:25;Matendo 4:12
Yesu alisema dalili yasiku zamwisho ni makristo wa uongo. Mathayo 24:24. " Maana watatokea makristo wauongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza yamkini hata wateule.
Wenye Imani potofu na Manabii wa uongo wanaweza kujulikana kwa matunda yao, bila shaka ni yale matunda ya utakatifu,mafundisho na utii wake katika maisha binafsi. Yesu alisema kwamba wale tu wenye kufanya mapenzi ya Baba Yake ndiyo watakaoingia “katika ufalme wa Mungu”.
Namna kuu ya kuwatambua manabii wa uongo ni kwa kutumia Neno la Mungu ambalo lipo ndani yetu; nasema “NENO LA MUNGU AMBALO LIPO NDANI YETU”na sio Neno la Mungu lililoandikwa katika kitabu kitakatifu yaani Biblia, kwakuwa wakati unapokutana na mafundisho ya uongo/udanganyifu kutoka kwa manabii wa uongo unapaswa kupima kwa kutumia Neno lililopo ndani yako.
Ukweli unapoletwa kwako USIUPINGE.Yesu yuko tayari kulisha moyo wenye njaa na kiu ya haki,peleka shinda zako kwake.Usikubaliane na mtu ambaye hayuko tayari kuisikiliza sauti ya Mungu.BIBLIA PEKEE INAMAJIBU YOTE .
No comments:
Post a Comment