Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki dunia
Image captionTshisekedi alikuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miongo kadhaa
Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84.
Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu.
DR Congo: Tshisekedi asafirishwa Ubelgiji kwa matibabuTshisekedi: Tutamuonyesha 'kadi nyekundu' rais KabilaUtata DRC; wapinzani wadai ratiba ya uchaguzi wa mwaka huuWatu 20 wauawa katika maandamano DR Congo
Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.
Image captionTshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRC
Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.
Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment