UN: Misaada ya chakula yahitajika haraka Yemen
Image captionWFP imetumia zaidi ya dola milioni 800 kusambaza chakula kwa nchi zenye migogoro
Umoja wa mataifa umesema kuwa fedha zisizotosheleza imepelekea kupungua kwa misaada ya chakula nchini Yemen huku maelfu ya watu wakikumbwa na njaa.
Shirika la chakula duniani WFP limesema hali ya upatikanaji wa chakula katika eneo hilo sio wa kuridhisha na juhudi za haraka zinahitajika.
Mkurugenzi wa WFP Ertharin Cousin amesema kuwa wamepunguza kiasi cha chakula kilichokuwa kinagaiwa kwa wahitaji ili kuweza kugawa kwa watu wengi.
Amewataka wahisani kutoa misaada ya fedha ili kuokoa maisha ya watu nchini humo.
Amesema kuwa watu zaidi ya milioni saba hawana chakula Yemen.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment