Monday, March 13, 2017
Makonda azindua barabara Jijini Dar es Salaam jana
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa.
Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.
Mwaka jana RC Makonda katika harakati za kutatua kero za wananchi alipewa kero ya barabara hiyo na yeye kuikabidhi kwa kampuni ya ukandarasi Grant Tech Company ambayo ilijitolea kuikarabati barabara hiyo kwa kiwango cha zege.
Akiongea katika makabidhiano hayo Operation Manager wa kampuni hiyo, Bw. Maswingo alisema anayofuraha kumkabidhi mkuu wa mkoa barabara hiyo ya kimometa 1 ambayo inaonganisha katika ya Kurasini na Kilwa Road ikiwa imejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na aina ya magari ambayo yanatumia barabara hiyo.
“Hii barabara aliizindua mkuu wa mkoa mwaka jana mwezi 12 na sasa hivi tunamkabidhi ikiwa imekamilika. Barabara hii ni kiungo muhimu katika eneo hili bila shaka itachangia kuchochote maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa ni barabara hii ni kiungo muhimu,” alisema Mwaswingo.
Kwa pande wa mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda alisema barabara hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa itawarahishia wafanyabiashara kutoa mizigo yao bandarini kwa urahisi.
Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini kwa miaka mitatu.
"Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita haijapita" amesema Makonda .
Makonda amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.
Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni ndoto ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda inaendelea kutimia.
No comments:
Post a Comment