KESHA LA ASUBUHI
ALHAMISI-MARCHI 2, 2017
*SUALA LA KUFA NA KUPONA*
*"Akasema,niache,niende,maana kunapambazuka,akasema,sikuachi,usiponibariki." MWANZO 32:26*
▶Akiwa katika zahama kuu ya maisha yake,Yakobo alienda pembeni kusali.Alikuwa amejazwa na kusudi moja lililomtawala kabisa-kutafuta badiliko la tabia.
▶Ilikuwa kwenye eneo pweke la kwenye milima,makazi ya wanyama wa porini na maficho ya wanyang'anyi na wauaji. Akiwa mpweke na bila ulinzi,Yakobo aliinamia nchi katika dhiki yake kuu....Alitoa sala yake kwa Mungu huku akilia machozi kwa uchungu. Ghafla akashikwa na mkono wenye nguvu. Akadhani kuwa adui alikuwa anataka kumuua na akajaribu kujikwapua kutoka mkononi mwa mvamizi.
▶Pale gizani,hawa wawili walipambana ili kupata ushindi.Hakuna neno lililotamkwa,lakini Yakobo alitumia nguvu zake zote na alijitahidi muda wote. Alipokuwa akipambana hivyo kwa ajili uhai wake,hisia ya hatia iliugusa moyo wake;dhambi zake ziliinuka mbele yake zikimtenga na Mungu. Lakini katika hali yake hii mbaya ya kutisha,alikumbuka ahadi za Mungu na moyo wake wote ukaelekezwa kusihi apate rehema.
▶Pambano liliendelea hadi karibu kuche,wakati huyu mgeni alipoweka kidole chake kwenye paji la Yakobo na akalemaa mara ile. Ndipo mzee huyu wa imani alipotambua aina ya hasimu zake. Akajua kwamba alikuwa katika pambano na mjumbe wa kimbingu na ndio sababu jitihada yake (Yakobo) ambayo haikuwa ya kawaida kibinadamu haikuweza kumpatia ushindi. Huyu alikuwa Kristo,"Malaika wa Agano",ambaye alikuwa amejidhihirisha kwa Yakobo. Mzee huyu wa imani sasa alikuwa amelazwa na akiugulia maumivu makali,lakini hakuacha kumshikilia....
▶Yule mgeni alisihi,"niache,niende,maana kunapambazuka",lakini Yakobo akajibu akasema,"sikuachii,usiponibariki". Kama huu ungekuwa ujasiri unaotokana na majivuno,ufidhuli,Yakobo angeangamizwa mara moja;lakini namna ya Yakobo ilikuwa ni uhakika wa ungamo la kutostahili,huku akitumainia uaminifu wa Mungu anayetunza agano.
▶Kile Yakobo alichokipigania kwa nguvu zake mwenyewe bila mafanikio aliweza kukipata kupitia kwa kujitoa nafsi na imani thabiti.
*TAFAKARI NJEMA, UBARIKIWE*

No comments:
Post a Comment