» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: MTAZAMO WA DAUDI NA MTAZAMO WA SAULI

USHINDI HATIMAYE- MTAZAMO WA DAUDI NA MTAZAMO WA SAULI
Mhubiri: Mchungaji David Mbaga

Mafungu: 1 Samwel 30:6; 1 Samwel 30:1;1Korintho 10:13;Rumi 8:37-39;Rumi 8:28

“Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.”(Rumi 8:37)

Unataka Mungu aziongoze hatua zako au unataka ujichagulie na kupita pasi kupata maelekezo yake?

Ikiwa unataka kufanikiwa unahitaji kubadili mtazamo wako; mtazamo wako ukiwa hovyo huwezi kufanikiwa . Badili kufikiri kwako uwe na fikra chanya na utafanikiwa kwani kila jambo hutegemea mtazamo wako maana kesho yako i mikononi mwako.

Daudi alifundishwa na Mungu mwenyewe vita, alikuwa akiingia katika ulingo wa vita na maadui wa kidunia; lakini Daudi alikuwa juu yao wote.  Daudi alijua siri ya ushujaa wake ni Bwana na kwamba vita ni vya Mungu.Lakini Sauli alikuwa mwoga wa vita.

Usikate tamaa, usivunjwe moyo ,jiamini, pambana na mwisho utashinda; njia ya mafanikio imejaa na vikwazo vya kufisha moyo kwa hiyo usikate tamaa. Lenga fikra zako kwenye mambo yatakayokusaidia kutimiza hatma yako. Ambatana na watu ambao watakusaidia kufikia ndoto zako.Mungu wetu ambaye si fotokopi tukimkabidhi mizigo yetu yote yeye ni mwaminifu kutupatia mlango wa kutokea.

Mungu hufanya kazi na wale watendao mema,achana na rafiki yeyote ambaye tabia yake huwa inakurudisha nyuma katika kufanikisha malengo yako.Ikiwa ni rafiki , familia  ndugu wa karibu nawe, kaa mbali nao kwa kutoshiriki tabia zao mbaya zisije zikabadili mtazamo wako chanya.

Kubali ukweli ikiwa una mawazo hasi hii itakufanya iwe rahisi kwako kubadilika na kuwa na mawazo chanya.Kamwe husimfurahishe shetani; Ikiwa tumemchagua  Mungu kuwa upande wetu na tumeweka tumaini letu kama Daudi alivyofanya, hakuna changamoto au tatizo linaloweza kutuogopesha. Hakuna jambo linaloweza kuzidi uwezo wa BWANA wa kuokoa.USHINDI HATIMAYE

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...