» » Sekta ya Nyama matatani nchini Brazil

Sekta ya Nyama matatani nchini Brazil


Brazil ni moja ya nchi zinazozalisha na kusafirisha Nyama kwa wingi dunianiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBrazil ni moja ya nchi zinazozalisha na kusafirisha Nyama kwa wingi duniani
Rais wa Brazil, Michel Temer, amezihakikishia nchi za kigeni kuwa , kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, haina maana kuwa bidhaa zake si salama.
Rais Temer amewaambia mabalozi kuwa nchi yake bado imeendelea kuzalisha nyama yenye ubora, ingawa kumekuwa na shutuma kuwa viwanda vyake vikubwa vitatu vimekuwa vikiuza nyama iliyooza kwa miaka mingi.
Serikali ya Brazil ina wasiwasi kuwa Marekani, China na nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kupiga marufuku kuingiza nyama kutoka Brazil baada ya shutuma hizo za kushtua zilizojitokeza siku ya Ijumaa.
Polisi nchini humo walifanya ukaguzi nchi nzima na kushutumu makampuni ya ufungaji nyama JBS, BRF na makapuni mengine madogo madogo kwa kuuza nyama isiyo salama, kuku na bidhaa nyingine za nyama.
Zaidi ya wafanyakazi 30 wa serikali waliokuwa na jukumu la kukagua vitendo hivyo wanachunguzwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles