» » Rais Magufuli amfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa

Rais Magufuli amfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa


Rais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madiniHaki miliki ya pichaIKULU DAR ES SALAAM
Image captionRais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amemfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa.
Rais Magufuli amefanya hivyo siku chache baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini. Hata hivyo, haijabainika iwapo kuna uhusiano kati ya ziara hiyo na kufutwa kwake Ntalikwa.
Rais Magufuli alifanya ziara hiyo kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti, juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo, ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli alishuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa, ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 2 Machi, 2017.
Rais Magufuli akiangalia jinsi magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halaliHaki miliki ya pichaIKULU DAR ES SALAAM
Image captionRais Magufuli akiangalia jinsi magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali
Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Rais Magufuli alimuagiza mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP - Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola, kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.
Akiwa bandarini hapo Rais Magufuli pia, alishuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje, ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonyesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu, wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...